DODOMA: Mwanafunzi ajinyonga baada ya kuchukizwa na matokeo ya mtihani

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
47797df6008d2f1cc8cd7b992314612b.jpg

Mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kizota Mjini Dodoma, Yasin Abdallah, miaka 13, amekutwa amejinyonga bafuni nyumbani kwao baada ya kuchukizwa na kufanya vibaya katika masomo yake

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, Ernest Kimoli amesema tukio hilo lililotokea Desemba 2 eneo la Kizota Relini Manispaa ya Dodoma baada ya baba mzazi wa mtoto huyo, Hassan Juma, miaka 53 kugundua kujinyonga kwa mwanaye saa 6.00 mchana

"Sababu ya kujinyonga ni kuchukizwa na matokeo mitihani yake,"alisema

Diwani wa Kizota, Jamary Ngalya, alisema mtoto huyo ambaye alizikwa juzi jioni, alianza kwa kuwaeleza wanafunzi wenzake Ijumaa kuwa atajinyonga

Alisema baada ya kutamka hayo, wenzake walimwambia wanakwenda kumweleza mwalimu, hata hivyo baada ya kuwasikia wenzake aliwaambia kuwa anatania hawezi kufanya hivyo

Mwalimu mkuu wa Shule ya Kizota, Juma Malecela Mwanafunzi huyo alihamia Oktoba kutoka mkoani Kigoma

"Katika matokeo ya kumaliza darasa la nne alikuwa wa 129 kati ya 132 inawezekana huko alikuwa anafanya vizuri." alisema.
 
Miaka 40 umri ambao alimzaa huyo mtoto mtu anakuwa bado ni kijana sana.
Ndio ni kijana, lakini kinguvu si sawa kwa umri huu katika kukabiliana na changamoto za utafutaji wa mahitaji yake.
Ina maana mtoto akifika 20 baba ana 60.....akhaaa!!!
Mtoto akiwa na 30 baba 70, uwiano 0 hapo.

Mie mwanangu nimemzaa nikiwa na 16, yuko form 3, nina uhakika wa kumlea na kuwaona mpaka vijukuu vyake.
We unadhani huyo atawahi kuviona, tena mtoto mwenyewe alikuwa wa kiume (r.i.p)?
 
MBEGU ALIKUPA NANI AU WALIKUSAIDIA MBONA ULIKUA BADO MTOTO
 
This is too much!! Mnakwenda mbali na mnakosea na unastahili kuchukuliwa hatua. Ndiyo lakini hapa umetukana. Unajua sheria wewe?
Mimi ndo sijaelewa au wewe mbona sijaona kosa hapo linalostahili kuchukuliwa hatua au huyo bwana ni ndugu yako???
 
Back
Top Bottom