Dodoma: Mwanachuo anaswa na TAKUKURU akijaribu kuhonga aongezewe ufaulu

omugabire

Senior Member
Jun 17, 2019
128
174
TAKUKURU mkoani Dodoma inatarajia kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa nne kwa makosa mbalimbali ya rushwa akiwemo mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya kwanza ya ualimu Chuo Kikuu cha St. John kwa kosa la kujaribu kutoa hongo ya Sh.900,000 ili aongezewe ufaulu yeye na wenzake sita.

======

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mkoani Dodoma, inamshikilia mwanafunzi wa mwaka wa tatu, katika chuo kikuu cha St John's mkoani humo, James Kwangulija kwa kosa la kujaribu kutoa hongo ya laki tisa kwa afisa mitihani ili asaidie kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wenzake 6.

Akizungumza leo Januari 7, 2020, Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, Sosthenes Kibwengo, amesema uwepo wa tabia ya baadhi ya wanafunzi kutoa rushwa katika masomo, unapelekea kuzalisha wasomi wengi wasiokuwa na uelewa katika taaluma zao, hivyo kutokuwa na sifa za kuajiriwa kwenye soko la ajira hapa nchini.

"Leo tunatarajia kuwafikisha mahakamani watu wanne kwa makosa mbalimbali ya rushwa, akiwemo James Kwangulija (27), mkazi wa Kikuyu jijini Dodoma, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya kwanza ya Ualimu katika chuo cha St John's kwa makosa ya kujaribu kutoa hongo ya laki 9 kwa afisa mitihani wa chuo hicho ili asaidie kuongeza GPA kwa wanafunzi wenzake 6" amesema Kibwengo.

Katika hatua nyingine TAKUKURU mkoani humo, itamfikisha pia mahakamani Rainer Kapinga, aliyekuwa Mganga Mkuu Wilaya ya Bahi, pamoja na Raymond Mhegele ambaye ni Afisa TEHAMA wa wilaya hiyo kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka yao.
 
omugabire,
Watu 6 laki 9!!? Hiyo akili au matope? Kwani katika hao sita hakuna wanafunzi wa kike!? Washauliwe waende wakasome Mzumbe sheria kama ni wazuri wa sura watafaulu tu.
 
Ndio elimu yetu hiyo, bongo bado sana usomi feki tu; sitasahau siku nimeingia kwenye ofisi moja chuo fulani cha umma DSM, nikakuta mwanafunzi anajaziwa maksi kwenye report yake, masomo ambayo alikuwa hajayafanya mwanzo, sasa huyo muhusika ni ndugu yake, akawa anamwambia somo fulani nikuwekee ngapi? jamaa anajibu weka fulani, na somo fulani nimekuwekea 50 zinakutosha? nikawa najiuliza hivi hawa viumbe hawaoni aibu kuna watu humu ndani! Yule mwanafunzi nae alikuwa wa course ya ualimu!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzembe course work huwa wanaongoza wasichana warembo tuu kitivo cha sheria main campus( Morogoro)
 
TAKUKURU mkoani Dodoma inatarajia kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa nne kwa makosa mbalimbali ya rushwa akiwemo mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya kwanza ya ualimu Chuo Kikuu cha St. John kwa kosa la kujaribu kutoa hongo ya Sh.900,000 ili aongezewe ufaulu yeye na wenzake sita.

======

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mkoani Dodoma, inamshikilia mwanafunzi wa mwaka wa tatu, katika chuo kikuu cha St John's mkoani humo, James Kwangulija kwa kosa la kujaribu kutoa hongo ya laki tisa kwa afisa mitihani ili asaidie kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wenzake 6.

Akizungumza leo Januari 7, 2020, Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, Sosthenes Kibwengo, amesema uwepo wa tabia ya baadhi ya wanafunzi kutoa rushwa katika masomo, unapelekea kuzalisha wasomi wengi wasiokuwa na uelewa katika taaluma zao, hivyo kutokuwa na sifa za kuajiriwa kwenye soko la ajira hapa nchini.

"Leo tunatarajia kuwafikisha mahakamani watu wanne kwa makosa mbalimbali ya rushwa, akiwemo James Kwangulija (27), mkazi wa Kikuyu jijini Dodoma, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya kwanza ya Ualimu katika chuo cha St John's kwa makosa ya kujaribu kutoa hongo ya laki 9 kwa afisa mitihani wa chuo hicho ili asaidie kuongeza GPA kwa wanafunzi wenzake 6" amesema Kibwengo.

Katika hatua nyingine TAKUKURU mkoani humo, itamfikisha pia mahakamani Rainer Kapinga, aliyekuwa Mganga Mkuu Wilaya ya Bahi, pamoja na Raymond Mhegele ambaye ni Afisa TEHAMA wa wilaya hiyo kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka yao.
Usikute ni mkakati wa "MAPOROPESA" katika harakati za KUBALANSI MZANI ule wa wao kutuhumiwa kuomba rushwa ya ngono...!!!
 
Back
Top Bottom