Dodoma: Mussa Assad(CAG), ahojiwa na Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, ripoti kukabidhiwa kwa Spika..

Assad anawindwa kwa sababu ya dini yake. Kina Sheik Ahad wapo tu wanashangilia spika kumwita Asad kwa amri!
 
Imeripotiwa kuwa alipokuwa akitoka kuhojiwa waandishi walizuiwa kumuhoji Prof. Assad (CAG)
Kwa kumbukumbu tulizonazo hatujawahi kumsikia Mo Dewji akielezea tukio la kutekwa kwake kwa mdomo wake mwenyewe (alizuiwa kusema chochote zaidi ya kumshukuru magufuli)

Hali kadhalika msanii roma mkatoliki na Dr. Ulimboka hawakuongea chochote baada ya kunusurika kifo walipotekwa!

Je wimbi la "KAA KIMYA" litakuwa sehemu ya "deal" la ku neutralize upupu wa Subwoofer?
(Kama hujaielewa hoja soma coments za wenzio)
 
CAG ni mcha Mungu,naamini kabisa hawezi kutishwa na kitu/mtu yeyote ndio maana anasisitiza "hekima na busara itawale kwenye mawasiliano" kwenda kwake kwenye kamati ni sababu ya kutii wito wa "kisheria" na sio "mtu"
 
Kamati ya Ndugai najua ishapigwa shule hadi imebaki midomo wazi.

Ripoti wataifungia kabatini au kuichoma moto kuepuka aibu endapo itavuja.

Kitendo hicho kinawafanya wamakataze CAG kuhojiwa na huenda washamuonya asihojiwe kabisa na asiseme chochote kama ilivyo kwa Pascal Mayalla
 
Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya bunge amesema CAG ameonyesha ushirikiano wa kutosha na kwamba vielelezo alivyowasilisha bado wanavifanyia kazi.

Mwenyekiti huyo amesema kwa mujibu wa kanuni wakimaliza uchunguzi wao watakabidhi ripoti kwa mleta shauri ambaye ni Spika wa bunge kwa hatua zaidi za kisheria.

Source ITV habari
Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom