Dodoma: Mussa Assad(CAG), ahojiwa na Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, ripoti kukabidhiwa kwa Spika..

Nchi iko kwenye BBC hard talk kwanza, mwacheni CAG apumzike, hatuwezi kuhandle matukio mawili kwa wakati mmoja jamani, there is a rule of the game on the ground.
 
  • Thanks
Reactions: cmp
Weee mkuu kuingia kwenye hiyo kamati ni sawa na kuingia jandoni; ukitoka jandoni husemi ulichofundishwa. Sioni kama prof atanena lolote kuhusu yaliyojiri kwenye kamati. Muulize mkuu mwenzako Pascal Mayalla mbona alivyotoka hajawahi kusema lolote kuhusu alichoambiwa huko kwenye kamati.
Pascal Mayala anajibu zuri zaidi
 
haya mahojiano yangekuwa mubashara ingekuwa poa sana

tuone maswali ya hovyo hovyo ya kamati, maana hapa watakuja jitangazia ushindi ili khali tunafahamu uwezo wao wa kuhoji, kuchambua na kufahamu mambo ulivyo mdg
 
Weee mkuu kuingia kwenye hiyo kamati ni sawa na kuingia jandoni; ukitoka jandoni husemi ulichofundishwa. Sioni kama prof atanena lolote kuhusu yaliyojiri kwenye kamati. Muulize mkuu mwenzako Pascal Mayalla mbona alivyotoka hajawahi kusema lolote kuhusu alichoambiwa huko kwenye kamati.
Itatolewa summary yakilichojadiliwa na wenye kamati yao basi.

Lakini mbona uganda na kenya mambo kama haya huwa mubashara kwenye luninga hata kesi kubwa huwa mubashara kotini Tanzania kuna nini au ndiyo ndagu ya CCM?
 
Weee mkuu kuingia kwenye hiyo kamati ni sawa na kuingia jandoni; ukitoka jandoni husemi ulichofundishwa. Sioni kama prof atanena lolote kuhusu yaliyojiri kwenye kamati. Muulize mkuu mwenzako Pascal Mayalla mbona alivyotoka hajawahi kusema lolote kuhusu alichoambiwa huko kwenye kamati.
Mbona Pascal Mayalla alishagusia japo kwa ni kwa juu juu kuhusu hiyo issue ya bungeni!!
 
Ndiyo sababu mie niliandika humu CAG Assad asiende kwa huyo kikaragosi bila kuhakikishiwa kwamba mahojiano yataonyeshwa LIVE na pia kuwa na Mwanasheria wake.

Wahuni hao wa maccm hawatabiriki kabisa! Sasa kikaragosi cha dikteta Ndugai anamzuia CAG Assad kuhojiwa na vyombo vya habari!!! ANAOGOPA nini!?

mahojianopic.jpg

Mdhibiri na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad
Kwa ufupi
Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge leo Jumatatu Januari 21, 2019 saa 8 mchana imemaliza kumhoji Mdhibiri na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge.”

Dodoma. Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge leo Jumatatu Januari 21, 2019 saa 8 mchana imemaliza kumhoji Mdhibiri na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge.”
Wakati CAG akiondoka saa 8:47 atika viwanja vya bunge, maofisa mbalimbali waliwazuia waandishi wa habari kumhoji chochote.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka amesema atawaeleza waandishi wa habari kilichojiri katika kikao hicho.
CAG Assad aliyeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, Desemba Mosi mwaka 2014 ameitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN) akiwa New York, Marekani alikokuwa akihudhuria mkutano.
Alitumia neno “udhaifu” wa Bunge alipokuwa akieleza sababu za kutofanyiwa kazi kwa ripoti zake ambazo zimekuwa zikibainisha ufisadi.
Soma Zaidi:CAG aanza kuhojiwa na kamati ya Bunge
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi
 
Dah..
Naona jamaa katumia hekima sana kwenda.

Cha ajabu eti taarifa zinasema sio Spika aliyemuita, ila ni kamati ya maadili iliyomuagiza Spika amuite kuhojiwa.
Kinachofuata hapo jamaa ni kuibuka mshindi tu, halafu soon Jiwe anaitisha shughuli ya kitaifa anamualika Assad na kumsifia mambo yanakwisha.

Ndugai ajiangalie sana.
Jiwe si mwanasiasa.
Atamharibia sana political carrier yake, na baadaye Ndugai ataonekana kama Spika aliyevurunda Tanzania.
Spika ajiangalie nini wakati alitumwa! Au ndiyo ile tengeneza tatizo tatua tatizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1001175
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof Mussa Asad amewasili bungeni, Dodoma kuitikia wito wa kufika katika kamati ya maadili

CAG tayari kwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kuhusu madai ya kudhalilisha Bunge, inadaiwa alisema bunge ni dhaifu.

UPDATES:1115HRS

View attachment 1000982
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad akiwa tayari amefika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge Muda huu mjini Dodoma kuhojiwa kufuatia kauli za kudhalilisha Bunge akiwa ziarani nchini Marekani.
C.
UPDATES: 1500H Kusema CAG Prof. Musa Assad aliyeteuliwa Jakaya Kikwete ni kutaka kuleta ufitini, kwa nini usisema aliteuliwa na Rais?
unamtaja Rais mstaafu ili iweje? Unataka kutuaminisha kuwa anahojiwa kwa sababu ni mteule wa Kikwete?
 
Back
Top Bottom