Dodoma: Mussa Assad(CAG), ahojiwa na Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, ripoti kukabidhiwa kwa Spika..

Habari hizi nimepenyezewa na mbunge mmoja kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania.

Inasemekana wabunge kwa mapenzi yao wameomba kupiga picha na alhaj Prof Assad kwa kile walichokiita kuwa mashahidi wa historia ya bunge kwa vizazi vijavyo.

Mbunge huyu ananijuza kuwa hata wajumbe wa kamati ya maadili ya bunge wametamani kupiga picha na CAG wakidai kuwa ni jambo jema na la kawaida kabisa katika kuimarisha mahusiano.

Nimejiuliza tu kama hata mwandishi nguli hapa nchini Pascal Mayalla alipoitwa na kamati wabunge walimsubiri wapige naye picha.

Ni hayo tu kwa uchache
Maendeleo hayana vyama!
Kupiga picha na mtu imekua big issue mpaka uje ufungue uzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari hizi nimepenyezewa na mbunge mmoja kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania.

Inasemekana wabunge kwa mapenzi yao wameomba kupiga picha na alhaj Prof Assad kwa kile walichokiita kuwa mashahidi wa historia ya bunge kwa vizazi vijavyo.

Mbunge huyu ananijuza kuwa hata wajumbe wa kamati ya maadili ya bunge wametamani kupiga picha na CAG wakidai kuwa ni jambo jema na la kawaida kabisa katika kuimarisha mahusiano.

Nimejiuliza tu kama hata mwandishi nguli hapa nchini Pascal Mayalla alipoitwa na kamati wabunge walimsubiri wapige naye picha.

Ni hayo tu kwa uchache
Maendeleo hayana vyama!
Sasa kupiga picha na paskali si kujitia nuksi maishani. wewe na kizazi chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata bunge lenyewe limechukua kumbukumbu
IMG-20190121-WA0008.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah..
Naona jamaa katumia hekima sana kwenda.

Cha ajabu eti taarifa zinasema sio Spika aliyemuita, ila ni kamati ya maadili iliyomuagiza Spika amuite kuhojiwa.
Kinachofuata hapo jamaa ni kuibuka mshindi tu, halafu soon Jiwe anaitisha shughuli ya kitaifa anamualika Assad na kumsifia mambo yanakwisha.

Ndugai ajiangalie sana.
Jiwe si mwanasiasa.
Atamharibia sana political carrier yake, na baadaye Ndugai ataonekana kama Spika aliyevurunda Tanzania.

Ajiangalie nini? Unajua nyie jamaa zangu tatizo lenu shule finyu.Uliambiwa Ndugai ndiye mwenyekiti wa kamati ?
 
mahojianopic.jpg

Mdhibiri na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad
Kwa ufupi
Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge leo Jumatatu Januari 21, 2019 saa 8 mchana imemaliza kumhoji Mdhibiri na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge.”

Dodoma. Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge leo Jumatatu Januari 21, 2019 saa 8 mchana imemaliza kumhoji Mdhibiri na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge.”
Wakati CAG akiondoka saa 8:47 atika viwanja vya bunge, maofisa mbalimbali waliwazuia waandishi wa habari kumhoji chochote.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka amesema atawaeleza waandishi wa habari kilichojiri katika kikao hicho.
CAG Assad aliyeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, Desemba Mosi mwaka 2014 ameitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN) akiwa New York, Marekani alikokuwa akihudhuria mkutano.
Alitumia neno “udhaifu” wa Bunge alipokuwa akieleza sababu za kutofanyiwa kazi kwa ripoti zake ambazo zimekuwa zikibainisha ufisadi.
Soma Zaidi:CAG aanza kuhojiwa na kamati ya Bunge
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi
 
Back
Top Bottom