Dodoma: Mmiliki wa Shule na Mkurugenzi Islamic Foundation akutwa ameuawa kinyama ofisini kwake

Status
Not open for further replies.

marybaby

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
3,250
2,000
Kwa Waislamu hasa wanaume Kuna tatizo unakuta mtu Ana wake wanne wanaishi marneo tofautibali mbali hivyo mwanaume aweza amua Leo atakuwa wapi akitoka kaxini au kwenye biashara zake.Kila mtu asipomuona anadhani atakuwa kwa mke mwingine Kumbe Mara ingine kaenda kwa mchepuko au kafa.

Kuna mmoja aliwahi pata ajali akalazwa hospitali hajitambui alikaa wiki mbili hakuna mke Wala mtoto.kutokea kumwangalia Hadi mwenyewe alipozinduka ndio akawataarifu kuwa Yuko hospitali

Kama huyo alikuwa na wake wengi hata hizo siku tano chache.Waislamu waige tu Wakristo usipoonekana nyumbani hata siku moja tu kazi unayo ripoti zitapelekwa kila msikiti utangaze kidume kilichochochea.Ripoti polisi zitakuwepo na kila mortuary picha ya kidume itatolewa kwamba ikitokea hiki kidume chenye picha hii mkakiona kimekufa kinaingia mortuary kifua mbele mtutaarifu hakijaonekana nyumbani toka jana
Sidhani km udini ni sababu,
Jukumu la mke ni kujua mumewe ameshindaje,ameshatoka kazini,amefika sehem husika na hata muda wa kulala utambue mumeo analala.
Uloyasema hapo ni wale wanawake wa kusema Mimi nu mke huyo Mume ataenda na atarudi mwenye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MAUBIG

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
998
1,000
MAUBIG,
Ina maana huyu Mkurugenzi tukio limemkuta Dar akapelekwa Dodoma akiwa mzima? Au hata Dar hakufika kumwakilisha Shekh wa Dodoma mbona inachanganya hii. Kwa kweli Polisi wana kazi ngumu sana.
Kwa mujibu wa kijana wake alikuwa Dar na alipaswa kurudi Dodoma lkn baada ya hapo hakuonekana na simu hazipatikani mpka maiti ilivyokutwa ofisini

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wazo Langu

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
1,379
2,000
Kafa kifo cha mateso.
Kukatwa uume, jeraha la kisu tumboni na kufungwa kamba ni dalili kwamba alikua anateswa kuhojiwa taarifa fulani, sidhani kama lengo lilikua kumkata uume ila wamekata kumpa mateso.

Na kuhusu kukaa siku tano huenda alikufa baada ya mateso hata siku mbili mbele.

Lakini je, hiyo ofisi haina majirani?Familia yake haikumtafuta?
Jengo halina Camera za Usalama?
Walinzi wa zamu wana taarifa gani?
 

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
6,428
2,000
Angepiga mkewe aliyejipeleka mwanaume huyo anamhusu Nini?

Kama huyo mwanamke alikuwa akimpenda huyo aliyechinjwa lazima atamripoti tu polisi au mashoga zake watatoa
Anaweza asiende polisi kwa hofu ya kuunganishwa na mauwaji pia hofu huenda mume hakuwahi mwambia labda alikuwa anafuatilia kimya kimya.
 

mosabiy

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,506
2,000
Ndiyo mkuu

Make tunatoa viashiria vya tukio yy anakana kwa nguvu zote. Kwa watz ukikuta mwamme kauwa na kakatwa uume au wamem-sodomize hivyo ni viashiria vya awali kwamba huenda source ya kuuawa kwake ni uzinzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
UNAELEWA MAANA YA DEFENCE MECHANISM. UNAWAJUA WATU WANAOITWA PROFESSIONAL KILLER?
 

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,431
2,000
Dah! Poleni Ndugu wa Marehemu na Waislamu Wote kwa ujumla na watu wote wenye kuguswa na msiba huo. Tumaini vyombo vya usalama kufanya kazi take vyema na kuhakikisha wauaji wametiwa nguvuni.

Sheikh wa Mkoa ambaye alikuwa awakilishwe akamatwe Mara Moja kwa mahojiano.
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,175
2,000
Rip Rashid Dalai namkumbuka mika ya 80 mwishoni na mwanzoni mwa 90 akiwa afisa wa polisi upande CID mjini Morogoro
Yaani watu wakikulia timing asee..yani pamoja na uCID,wakamkamata akiwa off guard,,,wachache Sana wenye machale Kama Jason Bourne
 

3 Angels message

JF-Expert Member
Aug 3, 2017
3,320
2,000
Inasikitisha sana poleni sana
Aliyeuawa ni baba wa jirani yangu inasemekana alikuwa dar kwenye kikao ambacho alitumwa kumuwakilisha sheikh wa mkoa wa Dodoma, baadaye mawasiliano na familia yake yakapotea ndo mchakato wa kumsaka ukaanza kwa kumshirikisha RPC wa Dodoma ambaye naskia wanafahamiana. Jana jioni jirani yangu huyu akaja kuniaga kwamba anaenda Dodoma kusaidia kumtafuta baba yake kwani mama yake kampigia simu huku analia wakashindwa kuelewana.

Baada ya kama dakika 40 hivi mke wake jirani yangu akaja kwangu kunipa taarifa za msiba kwamba baba mkwe wake amekutwa amekufa ofisini na kesho anajiaandaa kwenda na yeye msibani Dodoma. Yeye alipewa taarifa za msiba na mmewe ambaye alikuwa njiani kuelekea Dodoma.

Namie ndo napata kwa undani taarifa hapa Jf kwamba mzee yule ameuawa. Allah ampe kauli thabiti mzee wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom