Dodoma: Mmiliki wa Shule na Mkurugenzi Islamic Foundation akutwa ameuawa kinyama ofisini kwake

Status
Not open for further replies.

Nsoji go Nvaa

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
757
1,442
Ndugu Rashid Dalai, mmiliki wa shule ya kiislamu ya Zam zam iliyopo Dodoma na pia Mkurugenzi wa taasisi ya Islamic Foundation amekutwa amekufa ndani ya ofisi yake iliyopo ktk jengo moja na ofisi za Magazeti ya Serikali (Habari leo na Daily News) hapa Dodoma mjini maeneo ya Nyerere Square (karibu na bank ya NMB Mazengo).

Mwili wake umekutwa jana, Desemba 25 lakini inasemekana maiti yake imekaa takribani siku 5 mpaka ilipogundulika jana na kukuta mwili uko uchi wa mnyama huku akiwa na majeraha ya kisu tumboni na inasemekana ana majeraha kwenye uume na huku akiwa amefungwa kamba kwenye kiti.

Kanzu yake imekutwa imewekwa pembeni haina hata doa la damu.

Ikumbukwe mwaka huu maeneo ya Morena Hotel pia mfanyakazi wa TAMISEMI naye alikutwa kafa ndani ya gari eneo la parking.

Tunaomba sasa ulinzi uimarishwe na camera zifungwe majengo yote muhimu jijini Dodoma.

Development story:

Mamia ya wakazi wa dodoma na vitongoji vyake wamejitokeza kwa wingi kumzika sheikh rashid bura hii inaonyesha kweli alikuwa kipenz cha watu lkn ktk mikusanyiko ya watu maneno hayakosekani baadhi ya watu wanadai Siku ya jumapili alisafiri na basi la kimbinyiko kutoka dar kwenda dom,pia kuna tetesi kua mkurugenzi wa kwanza wa hio taasisi nae alikufa kifo cha kutatanisha ..hizi ni tetesi tu mwenye info zaidi aongeze nyama kuna watu wanauliza ofisi zikoje hizo ofisi ni haya majengo ya msajili kila mtu au taasisi wanakodi ofisi kila mtu chumba chake so vigumu sana kumonitor nani kaingia nani katoka mtu unaweza kuingia na kutoka bila kuulizwa hata wa kukuuliza hayupo ni jengo la kama ghorofa 3 hv kwa kweli liko very locally

Habari zaidi, soma:

 
Wahusika wa mauaji haya wasakwe ili wafikishwe ktk vyombo vya sheria kwa mauaji haya ya kikatili

Ila siku 5 auwawe taarifa zisitoke hata kwa familia au aliaga anaenda safari kwa hiyo hawakuwa na wasiwasi ila vipi kwenye jengo harufu maana siku hizo mwili ungeshaanza kutoa harufu kali ambayo kwenye hilo jengo wangeshahisi kitu.Mimi nahisi ni chini ya hizo siku 5.

Pole nyingi sana kwa familia, ndugu jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito Bwana awafariji sana na kuwapa matumaini kuwa ipo siku wataonana na mpendwa wao Kristo ajapo mara ya pili
 
Siku 5 mpaka ilipogundulika jana na kukuta mwili uko uchi wa mnyama huku akiwa na majeraha ya kisu tumboni na amekatwa uume wake lkn wameuacha unaninginia na huku akiwa amefungwa kamba kwenye kiti kanzu yake imekutwa imewekwa pembeni haina hata doa la damu

Jr
 
Status
Not open for further replies.
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom