Babu Kijiwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2010
- 4,830
- 4,726
Wenye taarifa kamili tujuzeni kuhusu tetesi hii
===========
Mkuu wa wilaya ya Chemba mkoani Dodoma amesurika kipigo jioni hii baada ya kudaiwa kuwatukana wananchi wa kijiji cha Mlongia.
Sakata hilo limetokea katika eneo la kijiji hicho kinachopakana na Wilaya ya Kondoa baada ya DC huyo kuwataka wananchi wasilime mashamba yao kwa madai kuwa eneo hilo la ekari 500 linamilikiwa na mwekezaji.
Baada ya mkuu huyo wa wilaya kudaiwa kuwatolea lugha chafu na kuamuru mwenyekiti wa kijiji hicho akamatwe, wananchi walijawa hasira na kuanza kuushambulia msafara wa mkuu huyo wa wilaya.
DC huyo amelazimika kukimbia baada ya gari lake kupigwa mawe na baadhi ya viongozi wa wilaya akiwemo mkiti wa halmashauri wakalazimika kuvalishwa hijjab na kutoroka.
=====
DC WA CHEMBA ANUSURIKA KIPIGO
Mkuu wa Wilaya ya Chemba-Dodoma, Simon Odunga anusurika kipigo kwa madai ya kuwakataza wananchi wa kijiji cha Mlongia kulima eneo ambalo linadaiwa ni la mwekezaji.
Kwa mujibu wa Mjumbe wa Baraza la Kijiji, Salum Ikanda, sakata hilo ni baada ya DC huyo kuwataka wananchi waondoke eneo hilo la ekari 500 mara moja ili kumpisha mwekezaji.
Tukio hilo liliambatana na mkuu huyo kuamuru Mwenyekiti wa Kijiji akamatwe jambo ambalo liliwafanya wananchi kujawa hasira na kuanza kuushambulia msafara wake.
DC Odunga alilazimika kukimbia baada ya gari lake kupigwa mawe pia baadhi ya viongozi wa wilaya akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri walilazimika kukimbia pia.
Chanzo: Mtanzania