Dodoma: Mkurugenzi wa Chemba atakiwa kujieleza TAMISEMI kwa kuchelewesha miradi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amechefuliwa na kitendo cha ucheleweshwaji wa miradi katika Wilaya ya Chemba huku akimwagiza Mkurugenzi kuhakikisha anampelekea maelezo ni kwanini wasichukuliwe hatua kwa uzembe huo.

Hali hiyo ilijitokeza leo wakati alipotembelea Miradi inayotekelezwa kwenye Wilaya hiyo ambapo kwa kiasi kikubwa hakufurahishwa na kasi ya ujenzi wakati maeneo mengine nchini imekamilika licha ya fedha kutolewa kwa wakati.

Waziri Jafo ameitaja miradi hiyo kuwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na bweni moja katika Shule ya Sekondari ya Chemba na Jengo la Utawala la Halmshauri ya wilaya hiyo ambayo hadi sasa haina maendeleo yoyote licha ya kutakiwa iwe imekamilika mwaka huu.

Aidha, alikataa kupokea taarifa kuhusu mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo ambayo inaeleza uwepo wa mapungufu ya fedha wakati Serikali imetoa Fedha yote bilioni 1.8 lakini wao wanasema bilioni 1.5.

“Nimezunguka nchi nzima lakini hapa Chemba mna hali mbaya na hiyo inasababishwa na baadhi ya viongozi kutojua changamoto za wananchi maana hapa kuna watoto wanahitaji huduma lakini ninyi hamfanyi kazi na ni dhambi kubwa mnafanya” amesema Mhe. Jafo.

Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt. Semistatus Mashimba na wakuu wa idara kuwasilisha kesho maelezo kuhusu kwa nini wasichukuliwe hatua kwa uzembe wakutokukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati na uzembe uliokidhiri.

“Chemba ni wazembe na mmecheza na fedha licha ya kwamba Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe magufuli ndio ametoa na hii inatokana na wengi wenu mmekulia kwenye mboga nane na hamjui changamoto za wananchi wa chini,”amesisitiza Waziri Jafo.

Waziri Jafo ameongeza kuwa hawezi kuhangaika kwa watu ambao hawana uchungu na wananchi na kwamba kuna viongozi wamepewa dhamana lakini hawajui matatizo.

Kuhusu ujenzi wa Bweni na shule alisema viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba hawapo makini na kazi kwani miradi mingi imedorora, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleoya halmashauri hiyo.

“kwa sababu haiwezekani hadi leo hamjakamilisha ujenzi wa shule na bweni ndio mmeanza msingi kwahiyo nataka maelezo kwanini serikali isifanye jambo kwa uzembe huo, ujenzi hospitali za wilaya wenzenu wamefanya mambo makubwa zaidi ya mliyofanya na sijaridhishwa na mmenipa taarifa ya uongo kwamba mmepokea Bilioni 1.5 badala ya bilioni 1.8 ni kosa kubwa.amesisitiza” Waziri Jafo

Kutokana na changamoto hizo, Waziri Jafo amemwagiza Katibu Mkuu TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga kuunda timu maalum ili kuchunguza matumizi ya fedha za miradi katika Wilaya hiyo na kazi hiyo ianze Januari mosi hadi 19 mwakani iwe imekamilika.

“Pia wachunguze nani alifanya uzembe na kwanini ziliingia kule na kurudi serikalini pia wachunguze mahusiano yaliyopo baina ya watendaji na wafanyakazi maana hakuna mahusiano mazuri Chemba ili itafutwe dawa ya kuondoa changamoto hiyo,”Amesisitiza Waziri Jafo
 
Naona mawaziri wanashindana kwa kiki kwenye vyombo vya habari!Watendaji kazi wanayo,wanainamisha vichwa tu na kusema ndiyo mzee hata kama ni hapana!

Nakumbuka Jafo alishawahi kumfokea na kumwambia anamwamisha kituo Meneja wa Tanroads Arusha kisa ameshindwa kuleta wananchi kwenye ufunguzi wa barabara!

Nikawaza sana,hivi kazi wa Meneja wa Tanroads ni kuleta watu kwenye ufunguzi au ni kusimamia vyema barabara?
Jamaa hata hakujibu kitu akawa kainama tu!Hawa wanasiasa washenzi sana!
 
Kwani wakuu wa mikoa hawaoni? Hawatumi taarifa ya jinsi miradi inavyokwenda huko tamisemi? Huyu Jafo unaweza kudhani anafanya kazi sana kumbe nikwamba hayuko systematic na hana delegation of power nzuri anazurura kilasiku mwenyewe na kufokafoka tuu alitakiwa mapema agundue kunamiradi haisogei na aawakemee kabla yakwenda! Kwani hii nchi miradi ya tamisemi nimingi kiasi gani mpaka ushindwe kuifatilia kila wakati?
 
Wakurugenzi ndiyo wateule wenye kazi ngumu sana awamu hii. Lkn ndiyo hawa hawa waliotumika kama toilt paper kunajisi uchaguzi.

Malipo ya dhulma huwa ni hapa hapa duniani.
 
Sasa ni mwendo wa kutafutana wachawi tu, mfumo wa serikali za mitaa umeharibiwa kwa kuteua wanasiasa kuwa wakurugenzi na kunyang'anya makusanyo ya halmashauri kwenda hazina.
 
Jafo naye amezidi, kelelee nyingi kweli lakini hakuna chochote kinachofanyika
Ulitaka yeye ndo aende akatekeleze miradi ndo uridhike au? Watu wanapewa fedha na serikali kutekeleza miradi wanazembea half unataka awachekeee?
 
Back
Top Bottom