Dodoma: Mbunge viti maalumu CHADEMA aibua upya sakata la Bunge Live

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Sakata la Serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni limeibuka upya, safari hii ukielekezwa kwa Rais John Magufuli

Hata hivyo, shughuli nyingi zinazomshirikisha Rais zimekuwa zikirushwa moja kwa moja jambo lililomfanya Mbunge wa viti maalumu (Chadema) Aida Khenani kuhoji sababu za kuzuia shughuli za Bunge kuonekana moja kwa moja

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Khenani alisema Shirika la Utangazaji Tanzania TBC linatumia kodi za wananchi lakini vikao vya wabunge waliowachagua havionyeshwi moja kwa moja kuwawezesha kufuatilia wanachozungumza wawakilishi wao.

"Hapo kuna tatizo ", alisema Khenani.

Alihoji kama tatizo ni gharama kama Serikali ilivyoeleza, inakuwaje pale Rais anapozungumza gharama zinapungua na Bunge linaporushwa moja kwa moja ndiyo zinakuwa kubwa.

Khenani aliungwa mkono na mbunge wenzake wa Viti maalumu (Chadema) Mariam Msabaha aliyehoji sababu za Bunge kuwa na hofu ya vikao vyake kuonekana moja kwa moja.


Wabunge hao waliungana na mtangazaji wa zamani wa Shirika hilo, Juma Nkamia (Chemba - CCM) aliyesema mwishoni mwa wiki kuwa shirika hilo limefika mahali pabaya hadi kuazima mitambo kwa watu binafsi kwa ajili ya kurusha matangazo ya ziara ya Rais Magufuli mkoani Mtwara.
 
Back
Top Bottom