Dodoma: Mbunge Kubenea apelekwa Zahanati ya Bunge baada ya kujihisi vibaya

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea amepelekwa katika Zahanati ya Bunge baada ya kujihisi vibaya.

Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema leo Jumatano kuwa, Kubenea amefika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili ya Madaraka ya Bunge na amewaeleza kwamba hali yake si nzuri.

Kutokana na hilo, amesema amepelekwa kwenye Zahanati hiyo na hali yake itakapoimarika atahojiwa na Kamati.

Mbunge huyo ambaye alipelekwa Dodoma kwa ndege leo asubuhi, jana Jumanne alisema alikuwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay wilayani Kinondoni akisubiri utaratibu wa safari hiyo ya kwenda kuhojiwa kama Spika wa Bunge Job Ndugai alivyoagiza.

NB:

Hivi kamati hii kwanini wasifanye kama Mahakama walivyo fanya kwa Yusuf Manji kwenda pale Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI kumsomea mashtaka pale alipo.

Kutolewa hospitali Agakhan Dar, matokeo yake huko anapokelewa anaishia kulazwa kwenye Zahanati.

Chanzo: Mwananchi
 
Muhuni tu huyo. Mh. Spika peleka wanakamati hapo Zahanati ili ahojiwe na kutoa maelezo. Akikutwa na hatia apewe adhabu inayostahili. Akikoswa na Hatia atolewe hapo Zahanati haraka sana kwa kuwa anaharibu rasilimali za Bunge na pesa ya walipa Kodi.
 
shubaaaaaaaaaaaaamittttt
 
Back
Top Bottom