Dodoma: Majina matatu ya wagombea wa nafasi ya Skauti Mkuu, yapitishwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika jijini Dodoma umepitisha majina matatu ya wagombea wa nafasi Skauti Mkuu ambayo yatawasilishwa kwa mlezi wa Chama hicho Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya uteuzi.

Akitangaza matokeo hayo Rais wa Skauti ambae pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amewapongeza wale wote waliogombea nafasi hiyo na kushinda na kuwataka kuendeleza mazuri ya skauti ambayo yamekwishafanyika.

Ametaja majina ya wagombea nafasi hiyo ya Skauti Mkuu yaliyopendekezwa kuwa ni Rashid Mchata, Nehemia Mchechu na Aron Kagulumjuli.

“Tunawapongeza sana kwa kupendekezwa na mkutano mkuu, na mimi kwa uaminifu napekeleka majina haya kama yalivyopendekezwa kwa mlezi ili ateue Skauti Mkuu,” amesema Prof. Mkenda

Pia Mkutano huo umechagua wajumbe wa Bodi ambao ni Elizabeth Mkwasa, Kenedy Nsenga, Juma Dossa, Jacqueline Kawishe, George Miringai, na Tabia Mohamed.

Prof. Mkenda ameitaka Skauti kuendeleza kazi nzuri iliyokwishafanyika ya kuijenga Skauti Tanzania na kuifanya kuwa imara zaidi na kwamba ili kufikia kiwango hicho ni vizuri kuendeleza tabia nzuri ya uadilifu na nidhamu.

Amesema kwa kuwa mchakato wa kumpata Skauti Mkuu unaendelea aliyepo sasa ataendelea na kazi na kuomba skauti kuendelea kushirikiana nae katika kipindi hiki ambacho atakuwa anahudumu.

Awali Waziri Mkenda aliileza Skauti Tanzania kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana matarajio makubwa kwao katika kujenga ukakamavu na uzalendo kwa vijana na kuwataka kushirikiana na kuifanya skauti kuwa imara.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Naibu Waziri Ali Abdulgulam Hussein amewapongeza wale wote walioteuliwa na kuchaguliwa na kwamba kazi iliyobaki ni kuhakikisha wanaijenga Skauti imara yenye misingi na uzalendo ndani yake.

Kwa upande wake Kamishna Mtendaji Skauti Taifa Bibi Eline Kitali amesema kwa sasa Chama cha Skauti kina wadhamini watatu ambao ni Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu Awamu ya pili, Dkt. Salim Ahmed Salim Waziri Mkuu Mstaafu, Mhashamu baba Askofu Gervas Nyaisonga na kwamba katika kuongeza nguvu amewasilisha pendekezo la nyongeza ya mdhamini Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu Awamu ya Nne jambo ambalo liliungwa mkono na skauti wote.

IMG-20220704-WA0008.jpg

Kura za wagombea zikihesabiwa mara baada zoezi la kupiga kura lilipokamilika wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti uliafanyika jijini Dodoma.

IMG-20220704-WA0009.jpg

Wagombea watatu wa Skauti Mkuu Tanzania waliopendekezwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kulia ni Rashid Mchata, Nehemia Mchechu na Aron Kagulumjuli.

IMG-20220704-WA0010.jpg

Wagombea wa ujumbe wa Bodi ya Skauti wakijitambulisha wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania jijini Dodoma.

IMG-20220704-WA0011.jpg

Rais wa Skauti Tanzania ambae pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) akitangaza matokeo ya wagombe ujumbe wa Bodi Skauti na mapendekezo ya wagombea Skauti Mkuu wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika jijini Dodoma
 
Mchechu kalambishwa asali bado haridhiki? Atatoa wapi muda wa skauti huku akiwa na majukumu mazito pale NHC? Na huyo cheusi mangara Kagulumjuli arudi kwao akalime mbaazi ni mtu wa hovyo sana
Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika jijini Dodoma umepitisha majina matatu ya wagombea wa nafasi Skauti Mkuu ambayo yatawasilishwa kwa mlezi wa Chama hicho Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya uteuzi...
 
Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika jijini Dodoma umepitisha majina matatu ya wagombea wa nafasi Skauti Mkuu ambayo yatawasilishwa kwa mlezi wa Chama hicho Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya uteuzi.

Akitangaza matokeo hayo Rais wa Skauti ambae pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amewapongeza wale wote waliogombea nafasi hiyo na kushinda na kuwataka kuendeleza mazuri ya skauti ambayo yamekwishafanyika.

Ametaja majina ya wagombea nafasi hiyo ya Skauti Mkuu yaliyopendekezwa kuwa ni Rashid Mchata, Nehemia Mchechu na Aron Kagulumjuli.

“Tunawapongeza sana kwa kupendekezwa na mkutano mkuu, na mimi kwa uaminifu napekeleka majina haya kama yalivyopendekezwa kwa mlezi ili ateue Skauti Mkuu,” amesema Prof. Mkenda

Pia Mkutano huo umechagua wajumbe wa Bodi ambao ni Elizabeth Mkwasa, Kenedy Nsenga, Juma Dossa, Jacqueline Kawishe, George Miringai, na Tabia Mohamed.

Prof. Mkenda ameitaka Skauti kuendeleza kazi nzuri iliyokwishafanyika ya kuijenga Skauti Tanzania na kuifanya kuwa imara zaidi na kwamba ili kufikia kiwango hicho ni vizuri kuendeleza tabia nzuri ya uadilifu na nidhamu.

Amesema kwa kuwa mchakato wa kumpata Skauti Mkuu unaendelea aliyepo sasa ataendelea na kazi na kuomba skauti kuendelea kushirikiana nae katika kipindi hiki ambacho atakuwa anahudumu.

Awali Waziri Mkenda aliileza Skauti Tanzania kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana matarajio makubwa kwao katika kujenga ukakamavu na uzalendo kwa vijana na kuwataka kushirikiana na kuifanya skauti kuwa imara.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Naibu Waziri Ali Abdulgulam Hussein amewapongeza wale wote walioteuliwa na kuchaguliwa na kwamba kazi iliyobaki ni kuhakikisha wanaijenga Skauti imara yenye misingi na uzalendo ndani yake.

Kwa upande wake Kamishna Mtendaji Skauti Taifa Bibi Eline Kitali amesema kwa sasa Chama cha Skauti kina wadhamini watatu ambao ni Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu Awamu ya pili, Dkt. Salim Ahmed Salim Waziri Mkuu Mstaafu, Mhashamu baba Askofu Gervas Nyaisonga na kwamba katika kuongeza nguvu amewasilisha pendekezo la nyongeza ya mdhamini Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu Awamu ya Nne jambo ambalo liliungwa mkono na skauti wote.
View attachment 2280726
Kura za wagombea zikihesabiwa mara baada zoezi la kupiga kura lilipokamilika wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti uliafanyika jijini Dodoma
View attachment 2280727
Wagombea watatu wa Skauti Mkuu Tanzania waliopendekezwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kulia ni Rashid Mchata, Nehemia Mchechu na Aron Kagulumjuli
View attachment 2280728
Wagombea wa ujumbe wa Bodi ya Skauti wakijitambulisha wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania jijini Dodoma
View attachment 2280729
Rais wa Skauti Tanzania ambae pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) akitangaza matokeo ya wagombe ujumbe wa Bodi Skauti na mapendekezo ya wagombea Skauti Mkuu wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika jijini Dodoma
Ni vizuri tukajua walijiunga na skauti mwaka gani na walifikia ngazi gani.
 
Hao wagombea wana CV zimeenea
Ngoja nikupe Cv ya Rashid Mchatta

MUHTASARI WA UZOEFU NA SIFA WA RASHID MCHATTA

Ndugu Mchatta ana zaidi ya miaka 22 ya uzoefu wa kufanya kazi katika mazingira ya taaluma mbalimbali katika usimamizi, elimu, benki, masoko ya fedha na Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano; na zaidi ya miaka 40 ya kujitolea katika Harakati za Skauti.

Ana digrii za B.Sc (1998) na M.Eng (2000) katika Mifumo ya Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Usimamizi. Amepata mafunzo ya Usimamizi wa Muendelezo wa Biashara, Mkaguzi wa Ubora wa ISO 19011, Usimamizi wa Miradi katika Prince2, Mshauri wa Uwekezaji aliyeidhinishwa na kuteuliwa (NOMAD), Mfanyabiashara wa Soko la Hisa aliyeidhinishwa, amefunzwa katika Utawala wa Biashara na pia amefunzwa katika Kozi ya Capstone ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) cha Tanzania.

Katika skauti, amepata mafunzo ya Kozi ya Mafunzo ya Awali kwa skauta (PTC), Kozi ya Juu ya uongozi wa Skauti (Wood Badge), kozi ya Mkufunzi Msaidizi wa Viongozi (ALT) na kozi za Mkufunzi wa Viongozi (LT). Kwa sasa anazo Shanga Tatu za Wood Badge.

Alianza safari yake ya kazi katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Tanzania, mwaka 2000, akiwa Mhadhiri Msaidizi. Baadaye mwaka 2001 alijiunga na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kama Mchambuzi wa Mifumo ya TEHAMA. Akiwa BOT, alikuwa bingwa wa uundaji na usimamizi wa Mfumo Mkuu wa Uhasibu wa Kibenki (CBS) na utekelezaji wa miingiliano yake mbalimbali kama vile Mfumo wa Ulipaji Hundi Kielektroniki, Mfumo wa Malipo wa Benki za Tanzania (TISS), Mfumo wa Uchakataji wa Noti na Mfumo wa Dhamana za Serikali. Vile vile alihusika katika uundaji na usimamizi wa Mfumo wa Usimamizi wa Mabenki Tanzania.

Mnamo mwaka wa 2005 alihamishiwa kwenye Taasisi ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), ambayo kwa sasa inajulikana kama Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, ambapo alikuwa sheer ya timu ya waanzilishi wa Menejimenti ya Taasisi hiyo akisimamia TEHAMA.

Julai, 2018 aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, nafasi ambayo anaitumikia kwa sasa.

Amekuwa mjumbe wa Bodi na Kamati za Uendeshaji mbalimbali za mashirika/miradi inayojulikana. Hivi sasa ni mjumbe wa Bodi ya Benki ya Azania kama Mkurugenzi Huru (Independent Director) na Mwenyekiti wa Kamati za Uendeshaji za Miradi ya Kilimo na Maji mkoani Kigoma inayofadhiliwa na Enabel, ya Ubelgiji.

Zaidi ya hayo, vile vile anajitolea katika Chama cha Skauti Tanzania, kwa sasa kama Mkufunzi Msaidizi wa Viongozi (ALT), ambapo awali aliwahi kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Skauti (2013 hadi 2018) na katika vipindi tofauti kama Kamishna Mkuu Msaidizi. Katika nyanja za Kimataifa katika Skauti, aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati ndogo ya Utawala Bora chini ya Bodi ya Skauti ya Ulimwenguni (2018-2020). Kwa sasa anahudumu kama Mwezeshaji /Mtathmini wa Kanda wa Viwango cha Ubora katika utawala bora katika skauti (GSAT) na Mshauri wa Utawala Bora kwa Kanda ya Skauti Afrika.

Amevishwa tuzo ya Medali ya Heshima (2021) na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia ana Tuzo za Dhahabu & Shaba za Miaka 100 ya Skauti Tanzania (2017). Vile vile ni Mwanachama daraja la Shaba wa Wakfu wa Skauti Afrika.

Ni mtu anayejituma na anapenda changamoto na anafurahia kuchukua maono na kuyageuza kuwa matokeo yenye uhalisia.
 
CV zimeenea! Mbona umetoa ya mtu mmoja tu.
 
Ni haki yangu ya kidemokrasia kuweka CV ya mtu ninayemjua
CV ya mtu haihusiani na demokrasia ya nchi, ni vizuri muhusika akupe CV yake badala ya wewe kujitungia, hata hivyo wewe si muhusika kwenye uteuzi wa wagombea aliyewateua ndiye anatakiwa aweke CV zao ili tujue vigezo vya uteuzi, usijipe madaraka yasiyokuhusu.
 
Back
Top Bottom