Dodoma: Maji yana harufu kama ya bleach kwa takribani wiki mbili

NZURI PESA

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
5,959
2,938
Habari wadau,kumekuwa na harufu katika maji ya bomba inayo fanana na harufu ya Bleach kwa takribani wiki 2 sasa katika mji wa Dodoma kwa wale tunao tengeneza dawa ya madoa au batiki mtakuwa mnajua harufu ya bleach ilivyo.Naomba watu wa DUWASA kama mpo humu mnijibu harufu iliyo katika maji ya bomba ni ya aina gani ya dawa?Ahsante
 
Watakuwa wameweka Chlorine kuuwa vijidudu... Sasa hivi si unajua kuna tishio la kipindu pindu?
Kumbuka kuwa dawa haiwekwi kiholela. DUWASA wana maabara zao, kabla ya kusambaza maji kwa mteja huyapima kuhakikisha hayana vijidudu hatarishi... Wakiyapima wakakuta kuna vijidudu ndipo huyaweka dawa... Vumilia mkuu...
 
Hiyo ni Chlorine - kama alivyosema mkuu hapo juu, ni njia ya kufanya maji yawe salama na maradhi na vijidudu
 
Habari wadau,kumekuwa na harufu katika maji ya bomba inayo fanana na harufu ya Bleach kwa takribani wiki 2 sasa katika mji wa Dodoma kwa wale tunao tengeneza dawa ya madoa au batiki mtakuwa mnajua harufu ya bleach ilivyo.Naomba watu wa DUWASA kama mpo humu mnijibu harufu iliyo katika maji ya bomba ni ya aina gani ya dawa?Ahsante
Dodoma kipindupindu kimenukia toka mwezi uliopita. Hiyo inaitwa residual chlorine inawekwa ikinge maji kwenye mfumo wa usambazaji japo ni sumu ikizidi. Nchi zilizoendelea nyingi zimeachana nayo.
 
Dodoma kipindupindu kimenukia toka mwezi uliopita. Hiyo inaitwa residual chlorine inawekwa ikinge maji kwenye mfumo wa usambazaji japo ni sumu ikizidi. Nchi zilizoendelea nyingi zimeachana nayo.
ahsante mkuu.Ila itabidi nitumbukie maabara kidogo
 
Umenikumbusha form 2 kwenye chemistry
Topic ya water treatment

Na form 3

Topic ya Chlorine gas uses zake
 
Back
Top Bottom