DODOMA: Mahakama yamuachia huru Kubenea, Polisi wamdaka tena

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Habari wanaJF,

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea mapema leo ameachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Dodoma.

Hata hivyo muda mfupi baada ya kuachiwa huru kwa Mbunge huyo wa CHADEMA Askari wa Jeshi la Polisi wamemkamata tena na kuna kila dalili za kfunguliwa kesi mpya

Kubenea yuko Kituo cha Polisi cha Mkoa wa Dodoma

======

Mahakama ya wilaya ya Dodoma, ilipanga kutoa hukumu ya pingamizi lililowekwa na wakili wa mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, katika kesi ya jinai inayomkabili katika mahakama hiyo.

Pingamizi hilo lilihusu nyongeza ya muda wa siku 60 zilizoombwa na serikali, baada ya muda awali kumalizika.

Katika kesi hiyo, Kubenea anadaiwa kumshambulia kwa mateke, ngumi na makofi, Juliana Shonza, mbunge wa Viti Maalum na sasa ambaye amepata Unaibu Waziri.

Upande wa mashitaka ulilleta maombi hayo kupitia kifungu cha 225 (4) (C) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20.

Wakili wa utetezi, Isaac Mwaipopo alipinga kuwasilishwa kwa maombi hayo kwa maelezo kuwa yameletwa nje ya muda na kumetumika kifungu kisicho sahihi.

Kwa mujibu wa wakili huyo, kifungu kinachorihusu maombi ya aina hiyo, ni 225 (4) (b).

Amesema maombi ya awali ya nyongeza ya muda yaliwasilishwa mahakamani, tarehe 4 Septemba mwaka jana na hivyo tokea wakati huo, hakuna maombi mengine yoyote yaliyowasilishwa ndani ya muda.

“Mheshimiwa Hakimu, leo ni siku ya 70 tangu serikali kuisha siku 60 za maombi ya serikali. Hivyo basi, maombi haya ya leo, yameletwa mahakamani kinyume na sheria na batili,” alieleza wakili Mwaipopo.

Aliongeza: “Mahakama ni chombo huru na hivyo haipaswi kusumbuliwa na visababu visivyo na msingi. Ninaomba mahakama yako imuachie mshitakiwa na kuifuta kesi hii.”

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi, James Karayemah, alipanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo, leo tarehe 18 Januari 2018. ambapo Mahakama Imemuachilia huru Kubenea.

Kubenea alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 5 Julai 2017.
 
Polisi wa dodoma!!!! Mungu anawaona, k
 
Kweli police ni tawi la ccm
 
Hakuna shida yoyote hata katiba ya nchi kuna sheria imewekwa Rais hashitakiwi akiwa madarak na baada ya kutoka...Hata wabunge wakifanya mambo ya hovyo ndani ya bunge hawashitakiw...N vzr kutafta tafsr ya sheria mahakani lkn sio kupeleka kwa mihemko.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom