Dodoma - Madereva wa wabunge waibua ufisadi wa wabunge` | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dodoma - Madereva wa wabunge waibua ufisadi wa wabunge`

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 23, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]
  Madereva wa wabunge wakiwa wameshikana mikono uonyesha mshikamano wao katika kutetea mikataba yao

  MADEREVA wanaowaendesha wabunge wawalipua wabunge hao wadai wanafanya kazi bila mikataba ya kazi huku wakilipwa posho kidogo wawafananisha wabunge na mafisadi .

  Madereva hao wamesema kuwa wabunge wamekuwa mbele kutetea madereva wanaofanya kazi hiyo hapa nchini kupewa mikataba wakatikwa upande wao wabunge hao wamekuwa wakiendelea kuwafanyia ufisadi kwa kutowalipa fedha zao wala kuingia mikataba ya kisheria. “Wabunge wetu wanaongoza kwa kuikosesha serikali mapato yake na ajira kwa vijana kupungua kutokana na baadhi yao kushindwa kutoa mikataba ya kazi wala kuwalipa mishahara ambayo serikali kupitiabunge ilipendekeza kwa ajili ya madereva wa wabunge toka mwaka 2008 .

  Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Dodoma leo na mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima kwa sharti la kutotaja majina yao madereva hao walisema kuwa mbali ya wabungehao kuendelea kuhubiri juu ya ajira kwa vijana na maslahi ya maderevaila wameshindwa kabisa kuwalipa madereva wao misharaha inayotakiwa kulipwa na badala yake fedha zinazotolewa kwa ajili ya madereva na bunge zimekuwa zikichukuliwa na wabunge hao na waokuishia kuwalipa posho isiyowawezesha kuendesha maisha yao.

  Kwani walisema kuwa sehemu kubwa ya wabunge hao wameanzakuendesha magari yao wao wenyewe baada ya kushindana na maderevawaliokuwa wakiwaendesha awali baada ya kushindwa kuwalipa mishahara na posho zilizobainishwa kisheria na ofisi ya bunge. Hata hivyo walisema kuwa suala hilo la wabunge kushindwa kuwalipa vizuri madereva si kwa wabunge wa CCM pekee bali ni wabunge karibuwote wakiwemo wa vyama vya upinzani ambao baadhi yao kwa sasawanajiendesha wenyewe baada ya kukimbiwa na madereva wao kwa kushindwa kuwalipa.

  Pia walisema matukio ya ajali kwa wabunge yamezidi kuongezekakutokana na wabunge hao kushindwa kufanya kazi na madeva na kuishiakuifanya kazi hiyo wao wenyewe na matokeo yake kutokana na mawazo ama kuwa na mambo mengi kichwani wamekuwa wakishindwa kuyamundu magari yao na kuishia kusababisha ajali za barabarani ambazo baadhi ya ajali hizo zimekuwa zikisababisha vifo ama ulemavu kwa wabunge hao. “Leo ukitazama hapa bungeni Dodoma utaona idadi kubwa ya wabungewanajiendesha wenyewe kama si mbunge kuwaendesha wenzake basi mbunge amekuwa akijiendesha mwenyewe na wapo wanaokuja na madereva hadi hapa Dodoma na baada ya hapo dereva amekuwa akipewa nauli ya kurudi jimboni na mbunge anaendelea kujiendeshamwenyewe kama njia ya kubana matumizi “

  Aidha walisema kuwa miongoni mwa madereva waliokosa ajira ni pamoja na wale waliokuwa madereva wa mawaziri na manaibu mawaziri ambao hawakurejea tena baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza mabadiliko ya baraza la mawaziri hivi karibuni ambapo mawaziri hao kwa sasa wamegeuka kuwa madereva wenyewe.

  Makamu mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Adam Said alisema kuwa sababu yawabunge wengi kukimbiwa na madereva ni kutokana na maslahi duniwanayoendelea kulipwa na kuwa hivi sasa baadhi ya wabunge baada yakukimbiwa na madereva wamelazimika kuwatumia ndugu zao kama njia ya kukwepa kuwalipa mishahara .

  Pia alisema maisha ambayo madereva hao wamekuwa wakiishi mjini Dodoma ni heri ya omba omba kutokana na wabunge hao kuwalipa kiasi cha shilingi 50,000 ama chini ya hapo na kutaka kuitumia kwa muda wawiki moja ama mwezi mzima jambo lililopelekea madereva hao kupangavyumba mtaani na kuishi katika chumba kimoja zaidi ya watatu kama sehemu ya kubana matumizi.

  Mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Juvenille Joseph alithibitisha madaia ya madereva hao na kuwa tayari uongozi wake umefikisha malalamiko ya madereva hao katika ofisi ya chama cha wafanyakazi mkoa wa Dodoma pamoja na ofisi ya spika wa bunge Anne Makinda ili kushughulikia madaihayo. Alisema kuwa kwa sasa wanakusudia kuitisha mkutano wa dharura wa madereva wote wanaowaendesha wabunge ili kuweza kuwa na msimamo wa pamoja katika kupigania haki zao na baada ya hao watawatumia barua wabunge ambao wanajiendesha wenyewe ili waweze kujiunga na chama hicho cha madereva wa wabunge .

  Kwani alisema kuwa katika barua iliyotolewa na ofisi ya bunge Novemba 3 mwaka 2008 barua yenye kumbukumbu namba FA.155/206/01/70 ikiwa na kichwa yahusu posho ya ubunge Malimbikizo July –Octoba 2008ilibainisha posho na mishahara hiyo. Joseph alisema kuwa posho ya mafuta lita 1000 kwa lita shilingi 2500 kwa wakati huo ilikuwa ni kiasi cha shilingi milioni 2.5 kwa mwezi , Matengenezo yagari asilimia 40 ya thamani ya mafuta ambayo ilikuwa ni milioni 1 kwa mwezi , posho ya dereva siku 10 kwa shilingi 30,000(vijijini ) ilikuwa ni shilingi 300,000 na posho ya mbunge siku 10 kwa kila atakazokuwepo kijijini kwa kila siku shilingi 45,000 ilikuwa nishilingi 450,000 huku mshahara wa dereva kwa mwezi ulikuwa ni shilingi 100,000 na kufanya jumla kwa mwezi kuwa bajeti ya shilingi milioni 5,115,000 kwa wakati huo.


  Ila pamoja na sasa posho za wabunge kupanga ila bado wabungewamekuwa wakiwalipa madereva wao kiasi cha shilingi 70,000 hadi 90,000 kwa mwezi fedha ambazo haitoshi kwa maisha ya sasa hivyokutaka fedha za madereva kuingizwa katika akaunti zao na maderevawote wa wabunge kuwa na mikataba ya kazi badala ya kuendelea kufanya kazi kirafiki na kindugu.

   
 2. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Wabunge mnaojiendesha hima mkajiunge na chama chenu cha madereva.
   
 3. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  hili nalo neno
   
 4. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Wabunge mliopo hapa jamvini toeni ufafanuzi
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Pesa wanazopewa na serikali kwa ajili ya kuwalipa mishahara madereva inaenekea wanazichakachua kununua kura na kujipongeza na vimwana wawapo Dodoma. Kumbuka madereva hawa ndio wanaotumwa kwenda vyuoni kuwachukua vijana kwenda kuvinjari nao pub.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa nini wabunge wepesi kuwqanyooshea vidole wengine lakini udhaifu unapokuwa upande wao wanafukiafukia?
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Imefika wakati bunge (utumishi wa bunge) waingie mikataba na madereva moja kwa moja ili kuwasaidia kulipwa stahiki yao na kwa muda muafaka!
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Binafsi namtazamo tofauti juu ya hili. Sioni sababu ya Wabunge kuwa na mikataba rasimi ambayo inatambuliwa na bunge kwa vile si wabunge wote wanaotaka kuwa na madereva wa kuwaendesha. Kuna wabunge wengi ambao hupendelea kuendesha wenyewe kwa sababu za msingi au wanazojua wenyewe na kadiri ya dhamiri zao.

  Kuwa na mikataba ujue mzigo atakayeubabe ni mwananchi kwa vile gharama nyingi za madereva zitajitokeza hata muda wa kumsubiria mbunge pale nje atahitaji posho kama wabwana zao wanavyodai.

  Serikali ifute taratibu za kutoa malipo ya mishahara ya wabunge, na badala yake mbunge mwenyewe akiona anahitaji driver na amwajiri na kufanya naye mkataba kama mtu mwingine ye yote binafsi anavyofanya anapomwajiri driver.
   
Loading...