Dodoma Kuna Pesa, huu ni ukweli. Nashauri nendeni mkafanye research, muda ndio huu

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
3,960
2,000
Dodoma hii ninayoishi mimi ni ngumu sana, kwanza maji bado changamoto pia nyumba za kupanga ni shida sana...

Hizi nyumba kipindi hiki ni shida ila itafika kipindi zitakosa watu maana wapangaji wengi ni wafanyakazi wa govt na Mara nyingi kundi hili hupenda kujenga,
Wafanyabiashara huu mji bado sana
 

jigili

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
328
500
Siku zote nimekuwa nikisikiliza Sana vijana wenzangu kukimbiza na muda na kuacha kulialia sana hasa humu mitandaoni.

Simaanishi watu wote mkaishi Dom, Ila namaanisha mkaangalie fursa huko. Mimi naishi dar Ila Kuna fursa nimezipata huko na hakika nimeona pesa ipo.

Sijui Sana kuhusu mikoa mingine Ila kwa dodoma Shahidi ni Mimi mwenyewe.

Inawezekana ni kutokana na kuwepo kwa taasisi nyingi za serikali kuwepo huko, yes inawezekana.

Nilikuwa huko.mwezi uliopita kwa ajili ya kufatilia tender kwenye taasisi moja, na hakika mambo yamekuwa vizuri.

Kama unaweza kupata tender ya mil 48, na ukatoa kila kitu ukabaki na faida ya mil 18 sio mbaya kabisa. Yes pesa inachelewa kidogo, si unajua taasisi nyingi wanapenda credit terms. Na hapo baada ya miezi tena miwili unapata tender nyingine Kama hii au zaidi ni poa sana.

Nashauri Kama una muda au una rafiki au ndugu huko nenda, kaa hata wiki fanya research, zunguka zunguka ulizauliza naamini Kuna fursa unaweza pata na ukapata pesa nzuri tu.

N.B;
Ilazo ni sehemu nzuri sana, hili eneo nimelipenda Sana.Ilazo papo vizuri, natamani kupata kiwanja huko mwenye kiwanja huko naomba mawasiliano pm. Ilazo nimepaelewa sana,
Hapo kwenye Ilazo nakushauri rudi na wakati wa masika kaangalie vizuri!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom