Dodoma: Kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa 2022, leo Mei 19, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,930
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango yupo Mkoani Dodoma akiwa mgeni rasmi wa WIKI YA UBUNIFU KITAIFA 2022

Anthony Mtaka, Mkuu wa MKOA - Dodoma

Tunawapongeza sana Wizara ya Elimu kuyaleta maonesho haya hapa Dodoma. Na sisi kama mkoa tumetoa fursa. Kwenye ubunifu ambao upo tayari kufanyiwa majaribio, Mamlaka za Serikali za Mtaa kwa maana ya halmashauri zetu na ofisi za serikali zilizo katika ngazi yetu ya mkoa, tupo tayari kutoa ushirikiano ili majaribio haya na taasisi hizi zinayafanya waweze kuya-practice kwenye ofisi yetu.

Kwa mabanda tuliyoyatembelea tumewapa fursa. Tumetembelea banda la Chuo Kikuu cha Mzumbe, nimeona kuna ubunifu mzuri sana kwenye sekta ya afya.

Gaudencia Kabaka, Mwenyekiti – UWT

Kwa niaba ya chama nawashukuru wote waliowezesha ubunifu huu ambalo ni suala muhimu katika elimu yetu. Kwasababu elimu bila ubunifu itakuwa ni elimu ambayo haileti matokeo chanya, hasa kuleta maendeleo.

Tunaamini matumizi ya ubunifu huu yatawafikia jamii ili kufikia Maendeleo Endelevu

Anthony Mavunde, Mbunge - Dodoma Mjini


Moja ya changamoto tulizo nazo ni kuwa vijana wetu wengi wanajishughulisha na shughuli zinazochangia kuharibu mazingira ili kutengeneza mkaa. Baada ya maonesho ya kwanza tuliwachukua vijana na kuwaunganisha na Jiji la Dodoma kwa ajili ya kupata mikopo ya asilimia 4 ili waweze kupata zile mashine za kutengeneza ile mikaa inayotumia uchafu na magogo ya miti kwa ajili ya kutunza mazingira yetu.

Maonesho haya yamekuwa tunayaunga mkono n ani ya muhimu sana.

Ubunifu huu lazima na sisi tuutumie kwaajili ya kuiendeleza jamii yetu katika maeneo mbalimbali. Yupo kijana amebuni mashine ya kupandia pamba ambayo inamfanya mkulima atumie saa moja kwa hekari moja tofauti na zamani ambapo ilikuwa masaa 11 kwa mkulima anayetumia jembe la mkono.

Ubunifu huu tukiutumia vizuri tunaweza kuendeleza jamii yetu katika Nyanja mbalimbali.
 
Back
Top Bottom