Dodoma: Kesho ndiyo kesho, Mama Samia anakalia kiti chamani. Wanaopanga kumkwamisha tumejipanga kuwakwamisha

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Niko hapa Dodoma kwa majuma kadhaa sasa. Niko kwa kazi maalum ya kichama: kuhakikisha bila kutisha kuwa Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anakuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa. Baada ya kumrithi Urais Magufuli, umefika wakati wa kumrithi pia Uenyekiti wa CCM. Kwa mikakati iliyosukwa kichama, Mama Samia atashinda kwa kishindo kuliko cha nyundo.

Mama Samia anapaswa kukamata mipini yote miwili: CCM na Serikali yake. Hakuna mbadala. Hakuna kinyume na hicho. Mama Samia yu tayari kutuhudumia kichama baada ya kuonesha makubwa na ya kuvutia kiserikali. Umefika wakati wake kujidai na kujimwaga kwenye viti viwili vya chamani na serikalini. Mama Samia anaweza kutuvusha kichama.Anaweza kufungua uwanja wa kisiasa wa kisasa usio na visa na mikasa.

Makada tumezimisi siasa. Tumemisi mikutano motomoto isiyo na watoto kutangaza mazuri ya chama na kuendelea kujiaminisha kwa wananchi. Makada tumejiandaa kujimwaga kama maboga kwenye uwanja sawa wa kidemokrasia zisizo na ghasia wala udhia tukitupiana vijembe vikali kama nyembe. Tumemisi siasa za majukwaani na mikutanoni badala ya kujibanza kwenye ziara za viongozi wa kiserikali.

Mama Samia, baada ya kesho, atafungua neema ya kidemokrasia. Sisi makada wazalendo bila magendo tunawaonya wote wanaopanga kumkwamisha kwa kuibuka na hoja zisizo na haja mkutanoni au kumnyima kura, tutawadhibiti bila ya mtiti. Tumejipanga kuwakwamisha na kuwaaibisha. Tupo tunaosubiri kuimarika kwa demokrasia baada ya kesho kupata Mwenyekiti mpya. Wapo wanaosubiri teuzi ili wapate mchuzi.

Ofisi ya Spika wa Bunge ilipokea taarifa ya CHADEMA kuwafukuza wanachama wake 19 'waliopewa' Ubunge!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Team Magufuli mpaka sasa hawaelewi wako ndotoni au! Baadhi wanajitahidi kubadilika na kuyazoea maisha mapya. Ila wengine bado wamekaza tu shingo, huku wakiamini bado Hayati anaishi na ana nguvu ile ile nchini!

Yaani hawaamini kabisa kama kile walichokipigania kuanzia mwaka 2015, hakipo tena!
 
Tunachoitaji ni usalama na security ya nchi yetu..!! Hizi demokrasia zenu mlizokaririshwa huko Maghailibi zitakuja kutupoteza siku moja.
Kwa hiyo udikiteta ndio unalinda usalama wa nchi?daaa!!huko chad, afrika ya kati , licha ya viongozi wao kuwa madikiteta, kuna usalama?achaneni na mawazo ya miaka ya 70!!huo usalama wa nchi bila kuwa na usalama wa raia una maana gani??yaani kipindi cha meko, uhai wa raia haukuwa na maana tena, huo ndio usalama unaozungumzia?sasa unapokuwa na kiongozi ambaye hana huruma na wananchi wake, ina maana gani?sana sana ni kuwapa maneno ya kuwakatisha tamaa tu.ACHA MUNGU AITWE MUNGU.
 
Team Magufuli mpaka sasa hawaelewi wako ndotoni au! Baadhi wanajitahidi kubadilika na kuyazoea maisha mapya. Ila wengine bado wamekaza tu shingo, huku wakiamini bado Hayati anaishi na ana nguvu ile ile nchini!

Yaani hawaamini kabisa kama kile walichokipigania kuanzia mwaka 2015, hakipo tena!
Hao malofa siyo timu Magufuli ni timu Tundu Lisu
 
Kwa hiyo udikiteta ndio unalinda usalama wa nchi?daaa!!huko chad, afrika ya kati , licha ya viongozi wao kuwa madikiteta, kuna usalama?achaneni na mawazo ya miaka ya 70!!huo usalama wa nchi bila kuwa na usalama wa raia una maana gani??yaani kipindi cha meko, uhai wa raia haukuwa na maana tena, huo ndio usalama unaozungumzia?sasa unapokuwa na kiongozi ambaye hana huruma na wananchi wake, ina maana gani?sana sana ni kuwapa maneno ya kuwakatisha tamaa tu.ACHA MUNGU AITWE MUNGU.
Narudia tena kusema hizi elimu mlizolishwa zitaenda kuathiri taifa letu..!! Hiyo Demokrasia na uo uozo wenu sijui ndiyo uouo ambao Twiter walizifunga kwa usalama wa Taifa lao, hapo mtu mmoj mmoj wanauana kila siku na askari wao..!!

Fanyeni yote ila msiendekeze hizo Demokrasia ambazo zitakuja kuwasambalatisha kama taifa, hakikisha nchi yako inakuwa salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom