Dodoma: Katibu Mkuu CCM akutana na Katibu Mkuu wa CNDD - FDD cha Burundi

Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo leo tarehe 10/06/2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Tawala Cha Burundi cha CNDD -FDD Ndg. Reverien Ndikuriyo. Mazungumzo hayo yemefanyika katika Ofisi za Makao za Makao Makuu ya CCM jjini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi aliambatana na watumishi wandamizi wa CCM. Sambamba na mazungumzo haya zawadi mbalimbali zimetolewa.

#ChamaImara
#kaziIendelee

IMG-20210610-WA0148.jpg

IMG-20210610-WA0158.jpg

IMG-20210610-WA0149.jpg
IMG-20210610-WA0150.jpg
IMG-20210610-WA0152.jpg

IMG-20210610-WA0153.jpg

IMG-20210610-WA0154.jpg
 
Hakuna chama/serikali ambayo huwa inayopambana kushobokea ( kujenga Diplomasia ) nchi nyingine kama Burundi.
 
Ukitaka kumuaa nyoka anza kumulika miguuni
Sasha ameahidi kukutana na wapinzani
Sasa kwa kua kuna miadi hio wangeanza kukutana makatibu wakuu wa vyama husika halafu baadae ndio rais anafuata
Sasa ni kinyume chake
Yaani katibu mkuu anakutanishwa sijui na mavyama ya wapi hayo.!?
Hayana ishu kwa mwananchi anaeijua nchi yake!
 
Huyu jamaa huwa hapendi yale manguo yao kama ilivyokuwa kwa bashiru na polepole,walikuwa wanayavaa hadi kwenye sherehe/misiba isiyohusiana na chama.

Ila hilo jicho la katibu mwenezi wa ccm mimi huwa silielewielewi vile.
 
Hao wawili machungu ya kuondokewa wanayo na yawachoma hadi kwenye mifupa.
 
Huko Burundi hiki chama kimeungana na Wasiojulikana wa huko na Sasa kinaitwa
CNDD-FDD- MBONERAKULE (hawa mbonerakule ndiyo wasiojulikana).

Ni sawa na hapa kwetu mwendazake angeendelea angekuja kufanya fusion ya ccm na wasiojulikana. Na ccm ingebadilika jina na kuitwa "CCM- Wasiojulikana"
 
Mkuu jina kamili la CNDD - FDD National Council for the Defense of Democracy – Forces for the Defense of Democracy.
 
Hii ndio wanatamka "Sien-dede-Efdede". Mitaa ya pale radio Deutsche Welle na wataalamu walioshuka duniani kwa sauti maalum za kutangaza kina Amidou, achana na hawa kina Joji Njogopa wa redio zetu.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo leo tarehe 10/06/2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Tawala Cha Burundi cha CNDD -FDD Ndg. Reverien Ndikuriyo. Mazungumzo hayo yemefanyika katika Ofisi za Makao za Makao Makuu ya CCM jjini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi aliambatana na watumishi wandamizi wa CCM. Sambamba na mazungumzo haya zawadi mbalimbali zimetolewa.

#ChamaImara
#kaziIendelee

View attachment 1814106
View attachment 1814270
View attachment 1814107View attachment 1814108View attachment 1814110
View attachment 1814111
View attachment 1814272
CHAMA BORA KABISA DUNIA NZIMA CHAMA TAJIRI AFRIKA
 
Hakuna chama/serikali ambayo huwa inayopambana kushobokea ( kujenga Diplomasia ) nchi nyingine kama Burundi.
Wana malengo yao Mkuu....leo utawaona kama wanashoboka,ila kuna siku utawaelewa. Wenzetu wanaakili sana. Ukute huo ni mkakati wao wa miaka kadhaa then waanze kujipenyeza kwenye uwekezaji wa maeneo ambayo sisi tunayaona hayana maana.
 
Back
Top Bottom