Dodoma: Kanisa la Tanzania Fellowship lafanya maombi kwa siku nne kumuombea Rais Magufuli

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
KANISA la Tanzania Fellowship linafanya maombi maalumu ya siku nne ya kumwombea Rais John Magufuli na watendaji wake kuweza kufanya na kusimamia maamuzi yatakayoweza kuleta maendeleo kwa Watanzania bila kujali itikadi yoyote ya kidini.

Dodoma Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Fellowship, Dk Godfrey Malassy amewaeleza waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa, maombi hayo maalumu yamelenga kuomba huruma ya Mungu kuwezesha viongozi kutekeleza wajibu wa kuhudumia wananchi.

Amesema pamoja na kuombea viongozi wamelenga kuombea ujio wa Makao Makuu Dodoma kuwa na nguvu ya Mungu ili maamuzi yatakayokuwa yanafanyika katika jiji la serikali yawe yenye neema na heri kwa Watanzania wote. “Ukizingatia hata mwenyewe Rais amekuwa na maombi ya kuwaomba Watanzania kumwombea ili aweze kufanikiwa mahitaji yake kwa ajili ya Taifa hili la Tanzania. “Pia ni imani yetu kwa siku hizi nne za maombi hayo pia yatasaidia kuvunja nguvu ya shetani ili zisiweze kutawala Makao Makuu ya nchi ambapo kwa hivi sasa serikali imeamua kuhamishia hapa Dodoma,” amesema Dk Malassy. Aidha amewataka Watanzania kuunga mkono yale ambayo serikali ya awamu ya tano yameweza kufanikiwa kwa kuyaombea ili yaweze kuleta mabadiliko kwa Taifa.

“Kuna mengi ya kuyaombea kama vile miradi ambayo tayari imeonekana na ile ambayo ipo mbioni kufanikishwa, ikiwemo ndege zinazomilikiwa na Shirika la Ndege la ATCL na ujenzi wa reli ya kisasa.” Katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Magufuli amefanikiwa kuimarisha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma pamoja na kukemea uzembe na kujenga ari ya kufanya kazi haya yote yanahitajika kuendelea kuombewa.

Askofu huyo, hata hivyo alitaja malengo mengine ya kufanya maombi hayo ni kuhakikisha pia Taifa linakia mafanikio ya kutimiza ndoto zake za kuwa na uchumi wa viwanda. Dk Malassy pia amewashauri watendaji wa serikali kuhakikisha wanajisimamia katika nafasi zao kwa uaminifu ili waweze kuaminiwa kama ilivyo kwa Rais ambaye anakubalika na Watanzania.
 
Mathayo 4:8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,9akamwambia, "Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu."10Hapo, Yesu akamwambia, "Nenda zako Shetani! Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake."

(walokole kuweni makini kwa maana mmiliki wa hizi falme za dunia ndio huyo hapo juu akijaribu kumtamanisha Yesu)
 
Ndio njia peke ya kula hela yake, maombi na kumsifia
 
Mathayo 6:17-18
Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
 
KANISA la Tanzania Fellowship linafanya maombi maalumu ya siku nne ya kumwombea Rais John Magufuli na watendaji wake kuweza kufanya na kusimamia maamuzi yatakayoweza kuleta maendeleo kwa Watanzania bila kujali itikadi yoyote ya kidini.

Dodoma Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Fellowship, Dk Godfrey Malassy amewaeleza waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa, maombi hayo maalumu yamelenga kuomba huruma ya Mungu kuwezesha viongozi kutekeleza wajibu wa kuhudumia wananchi.

Amesema pamoja na kuombea viongozi wamelenga kuombea ujio wa Makao Makuu Dodoma kuwa na nguvu ya Mungu ili maamuzi yatakayokuwa yanafanyika katika jiji la serikali yawe yenye neema na heri kwa Watanzania wote. “Ukizingatia hata mwenyewe Rais amekuwa na maombi ya kuwaomba Watanzania kumwombea ili aweze kufanikiwa mahitaji yake kwa ajili ya Taifa hili la Tanzania. “Pia ni imani yetu kwa siku hizi nne za maombi hayo pia yatasaidia kuvunja nguvu ya shetani ili zisiweze kutawala Makao Makuu ya nchi ambapo kwa hivi sasa serikali imeamua kuhamishia hapa Dodoma,” amesema Dk Malassy. Aidha amewataka Watanzania kuunga mkono yale ambayo serikali ya awamu ya tano yameweza kufanikiwa kwa kuyaombea ili yaweze kuleta mabadiliko kwa Taifa.

“Kuna mengi ya kuyaombea kama vile miradi ambayo tayari imeonekana na ile ambayo ipo mbioni kufanikishwa, ikiwemo ndege zinazomilikiwa na Shirika la Ndege la ATCL na ujenzi wa reli ya kisasa.” Katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Magufuli amefanikiwa kuimarisha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma pamoja na kukemea uzembe na kujenga ari ya kufanya kazi haya yote yanahitajika kuendelea kuombewa.

Askofu huyo, hata hivyo alitaja malengo mengine ya kufanya maombi hayo ni kuhakikisha pia Taifa linakia mafanikio ya kutimiza ndoto zake za kuwa na uchumi wa viwanda. Dk Malassy pia amewashauri watendaji wa serikali kuhakikisha wanajisimamia katika nafasi zao kwa uaminifu ili waweze kuaminiwa kama ilivyo kwa Rais ambaye anakubalika na Watanzania.
Unaambiwa kila kona ya nchi ni full maombo kumuombea rais mpendwa na mchapakazi wa nchi hii asilegee, akaze zaidi MAJIZI yanyooke.
Kaskazini, kusini, mashariki na magharibi kote wananchi wanamuombea rais Magu. Kweli wananchi wameridhishwa na huyu rais aliyeletwa na Mungu ma Mungu anaendelea kumsimamia.
 
Waangalie wasilete maafa zaidi. Siku nne mnaweza kusababjsha watu wakaongea wenyewe. Korosho zimebana. Tumwkmbee Raisi wetu apate afya njema
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom