diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
KANISA la Tanzania Fellowship linafanya maombi maalumu ya siku nne ya kumwombea Rais John Magufuli na watendaji wake kuweza kufanya na kusimamia maamuzi yatakayoweza kuleta maendeleo kwa Watanzania bila kujali itikadi yoyote ya kidini.
Dodoma Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Fellowship, Dk Godfrey Malassy amewaeleza waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa, maombi hayo maalumu yamelenga kuomba huruma ya Mungu kuwezesha viongozi kutekeleza wajibu wa kuhudumia wananchi.
Amesema pamoja na kuombea viongozi wamelenga kuombea ujio wa Makao Makuu Dodoma kuwa na nguvu ya Mungu ili maamuzi yatakayokuwa yanafanyika katika jiji la serikali yawe yenye neema na heri kwa Watanzania wote. “Ukizingatia hata mwenyewe Rais amekuwa na maombi ya kuwaomba Watanzania kumwombea ili aweze kufanikiwa mahitaji yake kwa ajili ya Taifa hili la Tanzania. “Pia ni imani yetu kwa siku hizi nne za maombi hayo pia yatasaidia kuvunja nguvu ya shetani ili zisiweze kutawala Makao Makuu ya nchi ambapo kwa hivi sasa serikali imeamua kuhamishia hapa Dodoma,” amesema Dk Malassy. Aidha amewataka Watanzania kuunga mkono yale ambayo serikali ya awamu ya tano yameweza kufanikiwa kwa kuyaombea ili yaweze kuleta mabadiliko kwa Taifa.
“Kuna mengi ya kuyaombea kama vile miradi ambayo tayari imeonekana na ile ambayo ipo mbioni kufanikishwa, ikiwemo ndege zinazomilikiwa na Shirika la Ndege la ATCL na ujenzi wa reli ya kisasa.” Katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Magufuli amefanikiwa kuimarisha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma pamoja na kukemea uzembe na kujenga ari ya kufanya kazi haya yote yanahitajika kuendelea kuombewa.
Askofu huyo, hata hivyo alitaja malengo mengine ya kufanya maombi hayo ni kuhakikisha pia Taifa linakia mafanikio ya kutimiza ndoto zake za kuwa na uchumi wa viwanda. Dk Malassy pia amewashauri watendaji wa serikali kuhakikisha wanajisimamia katika nafasi zao kwa uaminifu ili waweze kuaminiwa kama ilivyo kwa Rais ambaye anakubalika na Watanzania.