Dodoma: Jeshi la Polisi lamuita Cyprian Musiba kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kutaka kuuawa

Singidan

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
876
923
Muda huu maeneo ya Dodoma, inasemekana kuwa mtu mmoja anyefahamika Kama mwanaharakati, Cyprian Musiba, amekamatwa na Jeshi la Polisi Jijini humo kwa kosa la Kusambaza hanari ya kutaka kuuliwa katika magazeti bila kuripoti tukio Hilo katika Jeshi la Polisi.

====

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limemuita kwa mahojiano mwanaharakati huru Cyprian Musiba baada ya kutoa tuhuma mbalimbali za kutishiwa kuuawa

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Feb.24.2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema Musiba kupitia baadhi ya magazeti hapa nchini amechapisha taarifa za kulalamika kutishiwa kuuawa na baadhi ya wanasiasa .

Hivyo Kamanda Muroto ametoa Rai kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa habari za makosa ya jinai kwenye vyombo vya habari bila kujulisha vyombo vya dola na jeshi hilo limemuita Musiba kwa Mahojiano zaidi dhidi ya Malalamiko yake.

Credit: Faustine Galafoni
 
Muda huu maeneo ya Dodoma, inasemekana kuwa mtu mmoja anyefahamika Kama mwanaharakati, Cyprian Musiba, amekamatwa na Jeshi la Polisi Jijini humo kwa kosa la Kusambaza hanari ya kutaka kuuliwa katika magazeti bila kuripoti tukio Hilo katika Jeshi la Polisi.
Mbuzi wa bwana heri,shamba la bwana heri...basi tufanye yote ni heri tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afande Mroto amdaka Mwanaharakati huru Cyprian Musiba
FB_IMG_1582557127176.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli yuko chini ya ulinzi sehemu salama kabisa
Muda huu maeneo ya Dodoma, inasemekana kuwa mtu mmoja anyefahamika Kama mwanaharakati, Cyprian Musiba, amekamatwa na Jeshi la Polisi Jijini humo kwa kosa la Kusambaza hanari ya kutaka kuuliwa katika magazeti bila kuripoti tukio Hilo katika Jeshi la Polisi.
 
Haya labda ndo makubaliano na kina Membe au? Maana kikawaida hilo si kosa hata kidogo. Labda hao wanasiasa wawe wamelalamika polisi au maagizo kutoka juu.
 
Musiba ni nani zaidi ya mpiga filimbi ya Ccm? Tuna taka kusikia Lugola kaungana na kina James Ruge Segerea. Wasihamishe mada kwa stori za huyu Musiba.. We need to hear curruption ya kina Lugola imefika wapi? Maana Tz kwa kubadilisha mada Tuko powa
 
Back
Top Bottom