#COVID19 Dodoma: Hospitali ya Rufaa yaanza ufuaji wa Hewa ya Oksijeni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Wakati wakazi wa Dodoma nchini Tanzania wakitakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19, uongozi wa mkoa huo umesema hospitali zake hazijazidiwa na idadi ya wagonjwa.

Aidha, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma imeanza kufua hewa ya oksijeni ambapo kwa siku wana uwezo wa kuzalisha kati ya mitungi 250 hadi 300.

Hayo yamesemwa Julai 25 2021 na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best Magoma wakati walipotembelea hospitali hiyo wakiwa wameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.

Amesema pamoja na kuzalisha kiasi hicho cha hewa hiyo, wamesambaza mtandao wa hewa hiyo kutumia mabomba katika wodi ya watoto, upasuaji na ya wagonjwa mahututi (ICU).

“Uzalishaji huu umepunguza gharama za ununuzi wa hewa katika hospitali hii kwasababu si ya kununua ni ya kutengezwa…mmejionea pia vitanda vingi vitupu ni moja ya maandalizi ya kipindi hiki cha Uviko-19,"amesema.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk Ernest Ibenzi amesema pamoja na uwezo wa hewa inayozalishwa kuweza kuhudumia watu 200 kwa mara moja hawajawahi kufikisha idadi hiyo tangu waanze kufua hewa hiyo.

“Kwa mara ya mwisho kupata wagonjwa wengi wanaohitaji hewa ya oksijeni ilikuwa ni wagonjwa 29 tu kwa wakati mmoja,”amesema.

Kwa upande wake Mtaka amesema bila kutaja idadi ya wagonjwa waliopo wa Uviko-19 mkoani Dodoma katika hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Benjamin Mkapa.

“Wito wangu kwa wakazi wa Dodoma wasibahatishe akaona dalili akasema labda kikohozi hiki ama kikohozi hiki kinahusika na Covid. Kwenye upimaji inatusaidia zaidi sisi Serikali kuweza kujua kwamba hali ya vituo vyetu vya afya ikoje,”amesema.

Amesema bado wanajitosheleza katika hospitali na maeneo ya kutoa huduma na kuwatoa hofu wananchi kuwa hawajazidiwa na wagonjwa (overcrowed).

Chanzo: Mwananchi
 
Basi ni hatua nzuri, Tuzalishe mitungi mingi sasa tu supply kwenye hos zenye upungufu wa hewa...
 
Wakati wengine wanatumia kichwa, kuna wengine huwa wanatumia makalio..

Kongole kwa uongozzi wa hospital, mmetumia ndonga
 
Gaidi mbowe akisikia hivyo roho inamuuma sana, anataka tuagize mitungi nje ya nchi.
 
Hizo hospitali nyingine zenye upungufu nao waanze kufua hiyo Oxygen, wameshaamshwa usingizini.
 
Back
Top Bottom