Dodoma: Hatimaye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), yawasilishwa rasmi Bungeni

Mafisadi na wapigaji wazalendo naona mpango wao wa kuzuia ripoti isisomwe bungeni na kujadiliwa umebuma ,sijui wanapanga mbinu gani nyingine .
 
Kufuatia chagizo na presha kubwa ikiwa ni pamoja na matakwa ya kikatiba, leo tarehe 10 Aprili ikiwa ni siku ya mwisho kwa mujibu wa Katiba, Serikali imewasilisha Bungeni taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kama ilivyotakiwa. Orodha ya shughuli za Bunge leo inaonyesha taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) itawasilishwa bungeni.

View attachment 1067384

Kwa kufuatia hatua hiyo, Ofisi ya CAG sasa inaweza kuzitoa ripoti hizo katika tovuti yake ili Wananchi waweze kuzisoma na kuelewa fedha zao zimetumikaje. Ni suala la uwajibikaji tu, tunatoa heko kwa watu waliopiga kelele ili takwa hili la kikatiba litekelezwe.

Kwa upande wa Serikali, niwashauri wajifunze na waendelee kuheshimu Katiba. Kuna kikundi cha watu ndani ya Serikali kwa sasa wanampotosha kwa makusudi Rais ili wajipatie sifa , waache huo ujinga.

Kwa upande wa Bunge, nyie mmethibitisha kuwa dhaifu, wananchi hawana muda na Bunge kwa sasa, bora waangalie tamthilia ya SULTAN.

=======

Siku ya saba baada ya kuanza kwa mkutano wa 15 wa Bunge, chombo hicho cha kutunga sheria katika orodha ya shughuli za Bunge moja ya hati za kuwasilishwa ni taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, ambaye Aprili 2, 2019 Bunge lilipitisha azimio la kutofanya naye kazi kutokana na kukiita chombo hicho dhaifu.

Dodoma. Leo Jumatano Aprili 10, 2019 Bunge la Tanzania litawasilishiwa hati ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

Orodha ya shughuli za Bunge leo Jumatano, Aprili 10 inaonyesha taarifa hiyo ya fedha ya mwaka wa fedha 2017/18 itawasilisha bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisa ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ikiwa ni siku ya saba tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti Aprili 2, 2019. Hata hivyo orodha hiyo inaweza kubadilika.

Wakati taarifa hiyo ikiwasilishwa, jana Jumanne, Aprili 9 jioni ofisi ya CAG ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa leo Profesa Assad atakuwa na mkutano na waandishi kueleza yaliyomo katika taarifa yake ya ukaguzi.

“Nawakaribisha katika ukumbi wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (Naot) ghorofa ya pili. Jengo lipo nyuma ya jengo la hazina (Dodoma). Karibuni nyote msihofu,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ya mwaliko.

Hata hivyo, siku zote taarifa hiyo baada ya kuwasilishwa bungeni, CAG hukutana na wanahabari katika ukumbi wa Bunge kueleza yaliyomo katika ripoti yake ya ukaguzi, huenda safari hii ameamua kufanyia ofisini kwake kutokana na azimio la Bunge la kutofanya naye kazi.
Hivi Tamthiria y’a Sultan inaoneshwa Chanel gani?
 
Follow-up report on implementation of the CAG recommendation for the five performance Audit Reports issued and tabled to the Parliament in April, 2015.
Hii si Audit Report ya FY 2017/18!!!

Hiyo uliyoisema wewe ya April, 2015 inawasilishwa na Waziri Mkuu.

Sehem ya chini kuna report kuu ya mkaguzi 2017/2018 inawasilishwa na waziri ofisi ya rais, TAMISEMI.
 
Mkuu Terrible Teens, kwanza asante sana kwa hii. Pili samahani sana kuku doubt pale mwanzo, sasa nimekukubali sana. Tatu kiukweli JF tuna hazina kubwa ya watu, hizi pen names zinaficha mengi, kuna watu humu hatuwajui who they are the real ones, kumbe ni watu wakubwa, nyeti na watu wa maana sana. Heshima mbele.

Wito kwa wana JF Wenzangu, msimdharau mtu yoyote humu, huwezi jua nani ni nani!.
Big up jf, big up jf members.
P
Mpaka leo umeongea hivi inaonyesha mwanzo uliiona jf kwa jicho dogo saana.

Nikuambie tuu asilimia kubwa hata hawa viongozi unaowaona live na unaowajua amini tunapiga nao misele humu ndani,
Ndio maana jf ni dunia nyingine ambayo kuiishi ki uhalisia ni vigumu.

Asilimia tisini ya mtandao unaoogopeka hapa tz ni hii jf.

Nimewahi kumchungulia kigogo mmoja wa hapo magogoni yuko bize na simu, nilipomchungulia alikuwa anapitia jukwaa la siasa japo sikubahatika kujua alitaka aingie chumba kipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda walisema hawatafanya kazi na CAG ila watafanya kazi na makaratasi yake.

kwi kwi kwi kwi kwi bunge la maCCM
 
83 Reactions
Reply
Back
Top Bottom