digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 7,781
- 14,099
Ujenzi wa Msikiti wa Chamwino Mkoani Dodoma ambao Rais Magufuli aliahidi atashirikiana na Wananchi wengine kuujenga na akaanza kwa kuendesha harambee ya ujenzi wake akiwa Kanisani Chamwino, hatimaye umekamilika.
Itakumbukwa Jumapili ya August 23,2020 JPM alihudhuria Misa Takatifu na uzinduzi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata,Ikulu Chamwino, Dodoma, ambapo alisema Waislamu pia walichangia ujenzi wa Kanisa hilo na kuwataka na Wakristo kuungana na Waislamu kuchangia ujenzi wa Msikiti Chamwino kupitia harambee aliyoiendesha Kanisani hapo.
JPM alisema "Kwenye michango tuliyochangisha hapa Kanisani kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti Chamwino, tumepata jumla ya Tsh.Milioni 48 na Eflu 21, mifuko 48 ya cement na Lori 5 za mchanga, Rostam amechangia Mil 20, Bosa wa CRDB Nsekela Mil 10, pia CAG Kachere, Anthony Mavunde, RC Dodoma ni miongoni mwa waliochangia, sasa Msikiti utajengwa, Mimi nina Wasaidizi wangu wengine Waislamu yupo hai El Haji, wataswali kwenye Msikiti huo"
Twende na JPM 2020-2025