Dodoma: Fidia ya mashamba/viwanja ukanda wa kijani yajaa harufu ya dhuluma

BEYOND_LIMIT

Member
Feb 10, 2017
85
150
Kutoakana na mji wa Dodoma kuwekwa rasmi kuwa makao makuu imepelekea wakazi wa mji huo kuchukuliwa mashamba yao na serikali kwa fidia ambayo kiuhalisia inanuka dhuluma (kwa mtazamo wangu). Hii inatokana na namna fidia hyo inavyolipwa kwa watu wenye maeneo hayo ambayo mengi yao yalikuwa mashamba (katika eneo la kisasa karibu na chuo cha UDOM ambako inasemekana ni ukanda ambao utajengwa soko kuu, kiwanja cha mpira na stendi ya mabasi, kifupi ni sehemu ambayo iakuwa na fursa nyingi). Kwanin ninasema imejaa dhulma, ni kwa sababu zifuatazo:
 • Hakuna uwiano ulio wazi wa fidia ya mashamba hayo;
fidia inayotelewa ni mtu kupimiwa kiwanja katika maeneo mengine ambapo ukiangalia uwiano wake kwa kweli ni ukakasi. Mtu mwenye ekari 17 (Zaidi ya eneo la mita za mraba 68,000) za shamba anapewa kiwanja cha ukubwa wa eneo la mita za mraba 1500 kama fidia. Ukiangalia kwa uwiano huu tu utagundua mtu mwenye ekari moja ya shamba atatakiwa apate fidia ya kiwanja chenye ukubwa wa eneo la mita za mraba 88. Kwa huu uwiano hakika hapa kuna harufu ya wizi. Nimeweka picha za mgawanyo hapa.
 • Wahusika hawataki viongozi (walio teuliwa kwa upande wa wenye mashamba) wakae na wananchi kufanya vikao kujadili hatima ya mashamba yao kwa madai kwamba hitimisho limeshafikiwa.

 • Kuvunjwa kwa uongozi wa wawakilishi wa wenye mashamba bila kuhusisha wahusika (wenye mashamba)
Mimi sio mtaalam sana wa vifungu vya sheria lakini nina wasiwasi na mgawanyo huu huenda kuna watu wanataka kunufaika hapa.
Naomba mawazo/kufahamu sharia inasemaje kuhusu jambo hili kwa yeyote mwenye uelewa wa mambo haya.
 

Attachments

 • fidia.jpg
  File size
  120.1 KB
  Views
  24
 • upimaji.jpg
  File size
  170.8 KB
  Views
  21

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
4,883
2,000
Una uhakika haya malalamiko uliyoyaweka humu JF yatamfikia Mkurugenzi wa huo mji?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom