Dodoma: Daktari feki Hassan Abdallah, akamatwa katika hospitali ya Wilaya ya Chemba

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,739
2,000
JESHI la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mkazi wa Gairo mkoani Morogoro, Hassan Abdallah kwa tuhuma za kufanya kazi ya kitabibu pasipo kuwa na taaluma ya kazi hiyo.

Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Polisi Dodoma, Gilles Muroto amesema Abdallah anayetuhumiwa kuwa daktari feki katika hospitali za wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, alipohojiwa alisema anaipenda taaluma hiyo.

Kamanda Mulloto amesema mtuhumiwa huyo alikuwa anatoa huduma mbalimbali za upasuaji kwa wagonjwa wenye uvimbe, ambapo alianza kufanya upasuaji huo katika zahanati binafsi
“Tumemkamata akijihusisha na utoaji huduma mbalimbali za kitabibu na upasuaji mdogo kwa wananchi wenye uvimbe, tunaendelea kuchunguza kwa nini anafanya hivyo, tulipomhoji amesema alikuwa anafanya kwenye zahanati binafsi amekuwa akipenda taaluma hiyo ambapo anafanya hivyo pasipo kibali,” amesema Kamanda Muroto.

Kamanda Muroto amesema wanaendelea kumuhoji Abdallah na kwamba upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

“Tunamhoji tutamfikisha mahakamani. Hatuna nafasi ya utapeli kwenye mkoa wangu udaktari feki hauna nafasi, wananchi watoe taarifa za kutosha,” amesema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom