technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 12,495
- 50,965
----------Update----------
Mwenyekiti wa Bunge Mhe Chenge ameruhusu Bunge lijadili Hoja ya Mhe Waitara juu ya Kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kudharau Bunge.
Mhe Kadutu "Dharau za namna hii hazijawahi kufanyika. Hatuwezi kukubaliana na Viongozi wanaodharau Bunge"
Mhe Bulaya "Vijana wanaoaminiwa nasikitika wanatumia madaraka yao vibaya, wakuu wa mikoa, Wilaya"
Mhe Zitto "Bunge liazimie kwamba Kamati ya maadili iwaite na kuwahoji wahusike wanaotajwa kudharau bunge"
Mhe Kubenea "Ni lazima hadhi ya Bunge, heshima ya Bunge ilidwe kwa gharama yoyote".
Mhe Msukuma "Napendekeza kamati ya Uongozi iitishe kikao cha dharura kujadili kitendo cha Bunge kudharauliwa"
AG " Badala ya Bunge kuazimia kuwa wanaotuhumiwa wawajibishwe wahojiwe kwanza na Kamati ya Haki"
Mhe Chenge - Bunge limeazimia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru waitwe mbele ya Kamati ya Haki"