Anonymous
Senior Member
- Apr 6, 2006
- 116
- 336
Wabunge wawili Bashe na Musukuma wamekamatwa leo asubuhi kabla ya kikao cha Kamati Kuu kuanza kutokana na kudaiwa kubeba ajenda ya "kwenda kumpinga Mwenyekiti".
Kundi hili la wabunge lililokuwa na mjumbe mwingine, Adam Malima lilipanga Peter Serukamba ndiye awe kinara wa kuanzisha hoja ya kumpinga mwenyekiti.
Hata hivyo, kabla ya kutimiza azma yao walijikuta mikononi mwa Polisi huku Serukamba akidhibitiwa na kukosa kuwasilisha hoja ya kumpinga mwenyekiti, Magufuli.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibisha na kuwataja waliokamatwa kuwa ni Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe na Mbunge wa Geita vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma na Malima.
“Hao ndio waliokamatwa na bado tunaendelea na mahojiano na wengine bado tunaendelea kuwatafuta,”amesema Mambosasa.
Chanzo chetu kimedokeza kwamba huenda wakaendelea kushikiliwa hadi pale mkutano mkuu utakapomalizika!