Mtumishi wa Umma atakeyeteuliwa kwenye nafasi za kuteuliwa baadaye akatenguliwa nafasi aliyoteuliwa basi arejee kwenye mshahara ule wa awali kabla hajateuliwa.
Makes sense, mtu anatenguliwa lkn anaendelea kula same salary as yupo kwenye ile ile nafasi!!!
 
Kwa mara ya kwanza Rais wa mawe ametisha sana kaweka uzalendo mbele kwa kiwango kikubwa....sasa utekelezaji ufanyike isiwe maneno tu....
 
Pongezi kwa Dr. Mwigulu kwa kuwasilisha Bajeti ya kimkakati na yenye malengo ya kuchochea maendeleo ya nchi na wananchi.

Pongezi kwa Serikali ya awamu ya 6 , kwa umakini na weledi wa viwango vya juuu.

wananchi wanaona jinsi akili inavyo tumika zaidi kuliko nguvu.

kazi iendelee
 
Katika kutoa shukrani kwa nchi wahisani sijaisikia Urussi sasa haya mahaba kwa hawa mabwana yanatokea wapi?
 
Sio kwenye mshahara boss.
Inaonekana mkuu upo vizuri kiuchumi, Kwani ukiwa mfanyabiashara hujilipi mshahara?
Au mwenzetu ndio wale unachota tu na kutumia bila mahesabu?
Yote kwa yote budget ni nembo na mipango ya taifa lelote, usiidhihaki👏
 
Inaonekana mkuu upo vizuri kiuchumi, Kwani ukiwa mfanyabiashara hujilipi mshahara?
Au mwenzetu ndio wale unachota tu na kutumia bila mahesabu?
Yote kwa yote budget ni nembo na mipango ya taifa lelote, usiidhihaki👏
Nadhani unaongelea nadharia zaidi! Katika hali ya kawaida mtu binafsi hajilipi mshahara bali anatumia na kujibana kadri inavyowezekana!
 
Nadhani unaongelea nadharia zaidi! Katika hali ya kawaida mtu binafsi hajilipi mshahara bali anatumia na kujibana kadri inavyowezekana!
Utaratibu ni kujilipa mshahara huko kubana ni hulka au malengo ya mtu,
Kwani zikibaki kwenye matumizi ya mshahara si ni zako?
Au mwenzetu ni lazima umalize mshahara wote?
 
Kabla ya dhalimu kuingia madarakani na kuanza kuleta siasa za kiki, watu walikuwa wanavutiwa na bunge, na hata siku ya bajeti ilikuwa na mvuto. Ila alivyoligeuza bunge kuwa kibogoyo, na akanajisi uchaguzi wa 2020 hakuna mtu anayejitambua anafuatilia tena hilo bunge. Inshort hakuna mtu anafuatilia kinachoendelea huko bungeni, hivyo msome bajeti, msisome hakuna anayejali.
Mkuu wewe umekua,bajeti ya tz ni lini imekuwa msaada kwa raia?
 
Vipi bei za vinywaji vyetu pendwa??
Beer zimepanda bei au zimebaki vile vile??
 
.................Unaweza kukuta nchi ina wizara 25 lakini lakini ina Makatibu Wakuu 50 au zaidi
Unaweza ukakuta tuna halmashauri 184 lakini ukakuta tuna Wakurugenzi 300 au zaidi. Na hivyo hivyo kwa taasisi nyingine kwasababu waliotolewa wanaendelea kulipwa kama bado wapo ofisin....................

hii inchi inapitiaga wakati mgumu sanaa na ni vigumu kuelewa
 
Bajeti imekaa vizuri sana, jambo la msingi sasa ni kwa wabunge wetu wachangie mawazo ya kuboresha zaidi baadhi ya vipengele.

1. usimamizi wa fedha za Serikali ni jambo muhimu sana ili tija iweze kuonekana, udhibiti wa ubadhirifu, ufujaji n.k
nguvu kubwa iwekwe hapo.

2. Kubana matumizi yasiyo ya lazima.

3. Usimamizi wa miradi na kuona thamani ya fedha,
hayo yote yanawezekana endapo tu kila kiongozi atakuwa muadilifu ktk eneo lake.
tusioneane aibu.
 
Back
Top Bottom