TANZIA Dodoma: Asia Saidi, Mwenyekiti wa BAWACHA afariki dunia kwa kupigwa na mshale

Alfan issa

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,177
2,000
Duuh! tunakoelekea sio kabisa tukikoseana mtaan tunaanza kuwindana na mishale?

Pole kwa wafiwa
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,034
2,000
Asia Said Ali (50) Mrangi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA Kata ya Palanga, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kupigwa mshale na Mtu aliyefahamika kwa jina la Haruna Ali Kimata miaka 35.

Marehemu akiwa amekaa na mume wake muda wa saa mbili na nusu Usiku, Waliviziwa na Bwana Haruna Ali Kimeta kwa nia ya Kumpiga Mshale Mume wa Marehemu anayefahamika kwa jina la Iddi Masale miaka 55, lakini Mshale Ukamkosa na kumpata Mke wake Mgongoni ambaye alipoteza maisha Muda mchache baada ya kufikishwa Hospitali ya Kondoa.

Chanzo cha ugomvi, ni kwamba Iddi Masale aliingiza Mifugo kwenye Shamba la Alizeti la Haruna. Siku ya tukio, Mchana Walishinda Wanarumbana na kurushiana maneno Makali.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto ameiambia JamiiForums kwamba, Mtuhumiwa wamemkamata na Mshale uliotumika wameupata ambao ni kidhibiti na akaongezea kwamba, tukio hili halihusiani na Siasa.

Vita vikali sana, bahati mbaya Mama watoto imemuangukia yeye ilhali hana kosa.

Nilitamani Huu mshale ungelimpata huyu Bwana Mkubwa Muhusika alietia mifugo shambani kwa mwenzake.

Hawa Wafugaji wanajeuri sana ,
Wamezowea kusababisha Mgomvi ya sampuli hii kila mahali.

Mimi Binafsi Nina shamba mwaka wa 10 huu nashindwa kupata mavuno stahiki kwa vibweka vya wafugaji jinsi walivyo washenzi.

''Natamani na mimi nimiliki Nshale nintafute Ntu wangu anayenitenda kila Mwaka kwenye shamba langu.

Shenzi sana Hawa Wafugaji, sasa Kampoteza Mkewe kwa Ushenzi wake
RIP Mama watoto,
na Mumeo ndio muhusika mkuu,atawajibika kwa kukusababishia Mauti.
Poleni wafiwa.
 
zigii

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
516
250
Inawezeka vipi kumuua mtu kwa kumlenga shabaha mtu aliekaa na mwezake?
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,262
2,000
Jamani ungesoma habari yote hayo maswali yako ungejijibu mwenyewe bila kugusa key nyingi kivile.
🤣 🤣 🤣 🤣
Inaonyesha jinsi ambavyo unafikiri kama watu huwa hawasomi. Hiyo heading story imekuwa edited comment yangu ilikuwa na habari ambayo ni nusu nusu. Usiwe unakurupuka next time.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
105,687
2,000
Tutaamini vipi kuwa siyo la kisiasa?
Asia Said Ali (50) Mrangi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA Kata ya Palanga, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kupigwa mshale na Mtu aliyefahamika kwa jina la Haruna Ali Kimata miaka 35.

Marehemu akiwa amekaa na mume wake muda wa saa mbili na nusu Usiku, Waliviziwa na Bwana Haruna Ali Kimeta kwa nia ya Kumpiga Mshale Mume wa Marehemu anayefahamika kwa jina la Iddi Masale miaka 55, lakini Mshale Ukamkosa na kumpata Mke wake Mgongoni ambaye alipoteza maisha Muda mchache baada ya kufikishwa Hospitali ya Kondoa.

Chanzo cha ugomvi, ni kwamba Iddi Masale aliingiza Mifugo kwenye Shamba la Alizeti la Haruna. Siku ya tukio, Mchana Walishinda Wanarumbana na kurushiana maneno Makali.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto ameiambia JamiiForums kwamba, Mtuhumiwa wamemkamata na Mshale uliotumika wameupata ambao ni kidhibiti na akaongezea kwamba, tukio hili halihusiani na Siasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom