Dodoma: Ajali yaua Watatu akiwemo DAS Handeni

R.I.P

Ila magari ya serikali/yaliyobeba wakubwa huwa yanakimbia sana, tena bila kufuata sheria na utaratibu, unakuta kwenye kibao cha 50kms mtu anapita na 120km.

Sasa hapo mtu unabaki unajiuliza


Wapuuzi sana hawa wanawasha taa tu halafu anataka kuwasingizia Marehem. Kweli marehem hana haki..... yaan nimesikiliza maelezo ya huyo dereva nikajaribu kuwaza na uendeshaji wao nikasikitika tu.

Itakua hata kutoa kidogo kupisha basi hakutaka au alishindwa kutokana na mambio
 
kweli marehemu hana haki, lawama zimeenda kwa dereva wa basi wakati wao wanajisahau kwamba wana ruka na 120kph kwenye vibao vya 50kph wakidhani wana miili ya chuma ?, pumbav zao

anyway wapumzike pahala panapostahiki
 
Pumzika kwa amani kaka Maiga. Wana Mzumbe watakukumbuka enzi ulivyokuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi.
 
Hii gari inaonyesha ni Landrover discovery 3 or 4 automatic alikutana na kitu lazima maana rim na tairi bado nzima
Mkuu hizo gari ulizotaj hapo ni left handers??.

Maana kwa maelezo ya dereva hapo mbunge ambaye ni boss alikaa upande wa kulia pamoja na marehemu.
 
Watu Watatu wamefariki dunia akiwemo Katibu Tawala (DAS) wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Mwalimu Boniface Maiga Jumaa baada ya Gari mbili kugongana mkoani Dodoma usiku wa kuamkia leo.

Ajali hiyo pia imesababisha majeruhi kadhaa akiwemo Mbunge wa Handeni Mhe.Omary Abdallah Kigoda.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto amethibisha.

ITV BreakingNews
View attachment 1503466View attachment 1503467

DAS Handeni afariki Dunia kwa ajali ya gari
JUMAMOSI , 11TH JUL , 2020

Aliyekuwa Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Boniface Maiga amepoteza maisha katika ajali huku watu watatu wakijeruhiwa akiwemo Mbunge wa jimbo la Handeni Omary Kigoda ambaye amevunjika vidole viwili vya mkono wa kulia wakati wakielekea kwenye mkutano mkuu jijini Dodoma.



DAS%20WEB.jpg


Kwa mujibu wa taarifa yake Dereva wa gari la Mbunge wa Handeni Omary Kigoda, Peter Mganga amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa saba usiku katika eneo la Vikonji Dodoma.
Dereva huyo amesema chanzo cha ajali hiyo imetokana na mwendo kasi aliokuwa nao dereva wa basi baada ya kuovateki sehemu yenye kona.
Dereva huyo wa Mbunge amesema baada ya dereva wa basi kuovateki katika eneo hilo lenye kona kali alimuwashia taa ili aweze kupunguza spidi ya gari ila dereva wa basi hilo hakupunguza spidi na ndipo wakavana uso kwa uso.
''Katika ajali hii dereva na kondakta wa basi wote wamefariki nilijaribu kumuwaahia taa nyingi ili apunguze spidi lakini cha kushangaza kama hajaziona ilibidi sisi tupaki pembeni ndipo mwendo aliokuwa nao ililazimu kulivaa gari letu hasa upande wa kulia aliokuwa amekaa mheshimiwa Mbunge na Das wetu aliyefariki,''amesema Mganga.
MAGUFU21.jpeg

Amesema mara baada ya ajali hiyo Das alipoteza maisha hapo hapo huku wao wakikimbizwa katika hospitaliti ya Chamwino kwajili ya matibabu ambapo Mbunge alilazimika kufanyiwa upasuaji wa vidole hivyo wakahamishiwa katika hospitali ya Mkoa Dodoma (General Hospital).
Mganga amesema baada ya kupata matibabu wawili waliruhusiwa kutoka hospitalini hapo saa kumi na moja alfajiri huku Mbunge Kigoda akibaki kuendelea na matibabu ya vidole alivyoumia.
DAS1.jpeg

Amesema katika gari hiyo ya Mbunge Kigoda walikuwa watu wanne akiwemo yeye Dereva wa Mbunge Peter Mganga, Mbunge Omary Kigoda, Mbelwa Saidy ambaye ni ndugu yao pamoja na Boniface Maiga (DAS) aliyepoteza maisha na kueleza kuwa mwili wa marehemu upo katika hospitali hiyo ya Mkoa.
Aiseee yule das aliongea vizuri sana clouds hili ni pigo
 
Bora kafa na afe tu na huyo aliyewekwa hapo general hospital jifanyeni mko weekend. Wajinga sana. Manina wakufe tu ccm manina zao
 
Dah Mungu amlaze marehemu mahala pema peponi. Alikuwa rafiki yangu sana na alikuwa na haiba ya uongozi
 
Back
Top Bottom