do you rmbr this?Je wajua kuwa bdo lipo mahakaman?

Sir_Finus

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
330
139
Jaji katika kesi ya kwanza kabisa ya
kiraia dhidi mfungwa kutoka gereza la
Guantanamo, ametoa uamuzi kuwa
shahidi mkuu kutoka serikali ya
Marekani hatotoa ushahidi. Hatua hiyo ni pigo kwa waendesha
mashitaka. Mshukiwa huyo Ahmed Khalfan
Ghailani anakanusha kusaidia kundi la
Al Qaeda kufanikisha mauaji ya watu
224 mwaka 1998 katika balozi za
Marekani zilizoko Afrika Mashariki. Jaji huyo ametoa uamuzi kuwa shahidi
huyo wa serikali hatotoa ushahidi,
kwa sababu Bw. Ghailani alimtaja
shahidi huyo wakati akiwa "chini ya
vitisho". Mwandishi wa BBC anasema hatua
hiyo inazidi kuongeza ugumu katika
mipango ya kutaka kuwashitaki
washukiwa na Guantanamo katika
mahakama za kiraia. Utawala wa Rais Obama una
matumaini ya kuendesha kesi hizo
kwa washukiwa kadhaa, hasa wenye
'majina makubwa', akiwemo Khalid
Sheikh Mohammed anayetuhumiwa
kupanga mashambulio ya Septemba 11 nchini Marekani. Vitisho Jaji Lewis Kaplan wa New York
ameahirisha kesi ya Bw. Ghailani
iliyokuwa ianze kusikilizwa
Jumatano.Kesi hiyo sasa iko katika
hatua ya kutafuta wazee wa
mahakama itakayofanyika Oktoba 12. Katika uamuzi wake, jaji huyo wa New
York amesema shahidi huyo wa
serikali aliyependekezwa, alitajwa
katika "taarifa alizotoa Ghailani kwa
CIA wakati akiwa katika vitisho". Mtu huyo, Hussein Abebe, alitarajiwa
kutoa ushahidi kuwa alimuuzia
Ghailani milipuko ya TNT, ambayo
ilitumika katika mlipuko wa bomu
katika ubalozi wa Marekani nchini
Tanzania, mwezi Agosti mwaka 1998. Uamuzi huo, iwapo hautabatilishwa, ni
kikwazo kwa kesi ya serikali ya
Marekani dhidi ya Ahmed Khalfan
Ghailani, na pia hatua hiyo kutatiza
zaidi sera ya utawala wa Obama wa
kuwashitaki washukiwa wa Guantanamo katika mahakama za
kiraia. Shahidi mkubwa Hussein Abebe alitarajiwa kutoa
ushahidi. Bila ya shahidi huyo kutoa
ushahidi wake, serikali itapata tabu
kuwasilisha ushahidi wake mbele ya
wazee wa mahakama. Hatua hiyo
inawapa waendesha mashitaka tatizo kubwa -- iwapo ushahidi uliopatikana
katika magereza ya CIA au gereza la
Guantanamo hauwezi kutumika
katika mahakama ya kiraia, je kuna
uwezekano wa kukuta mshukiwa na
hatia?. Mwendesha mashitaka mmoja wa
Marekani amemuelezea Bw. Abebe
kama shahidi "mkubwa" kwa serikali,
na wanafikiria kukata rufaa dhidi ya
uamuzi wa jaji. Bw. Ghailani, ambaye inaaminika umri
wake ni kati ya miaka thelathini na
arobaini , alikuwa amevaa sweta la
rangi ya kijivu, suruali nyeusi na tai,
wakati alipofikishwa mahakamani,
siku ya Jumatano. Kifungo cha maisha Bw. Ghailani anatuhumiwa kununua
gari la milipuko iliyotumika katika
shambulio nchini Tanzania, na pia
kutuhumiwa kuwa mjumbe wa Osama
Bin Laden. Anakanusha mashitaka
hayo. Bw. Ghailani aliyekamatwa nchini
Pakistan mwaka 2004, alipelekwa
kisiri katika kituo kimoja cha CIA
kabla ya kupelekwa Guantanamo
mwaka 2006. Bw. Ghailani anakabiliwa na kifungo
cha maisha jela, iwapo atakutwa na
hatia.
 
Haisaidii, roho na damu za watu zaidi ya 200 haziwezi kwenda hivihivi, haki itatokea kwa mkono wa mungu.
 
Back
Top Bottom