Do what's right. Even if no one is watching

Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
16,426
41,526
Katika nchi ya ahadi, kulikuwa na kijiji chenye watu wenye furaha sana kilichoitwa JamiiForums. Hawa watu walikuwa na upendo mkubwa sana kati yao, na hata kwa majirani.

Siku moja wanakijiji wakaletewa taarifa kuwa kijiji cha jirani kilikumbwa na ukame uliopelekea kuibuka kwa njaa. Kama ilivyo desturi ya wanakijiji wa JamiiForums, wakakubaliana kuwasaidia majirani zao. Ukaitishwa mkutano wa kijiji ili waweze kujadiliana namna gani wafanye.

Mkutano uliisha kwa kukubaliana kuwa kila mwanakijiji apeleke lita 5 za maziwa. Na walipendekeza maziwa yote yakusanywe kwenye pipa la kijiji, lililopo nje ya nyumba ya Mzee wa Kijiji, Mr Analyse

Kesho yake mwitikio ulikuwa mkubwa sana. Hakuna mwanakijiji ambaye hakuonekana, na hakuna ambaye hakuleta maziwa. Yote kwa pamoja yalimiminwa kwenye lile pipa.


Mpaka inafika mchana, pipa lilikuwa tayari limeshajaa.

Wakateuliwa watu wachache kupeleka salamu za pole, pamoja na lile pipa la maziwa.

Salamu zilifika, na Wawakilishi wakaomba kile kidogo walichopeleka kipokelewe, na kikapokelewa.

Wale wanakijiji cha pili walipoanza kuchota kwenye lile pipa, walikuta maji (wakafurahi sana maana hawakujua ni zawadi gani walipewa). Wakashukuru sana na kuwaombea dua njema wanakijiji cha JamiiForums.

Wale wawakilishi walioteuliwa kupeleka salamu na lile pipa la maziwa wakashangaa sana kuona pipa lina maji. Mmoja akamuuliza mwenzake "Mbona ni maji badala ya maziwa?". Mwenzake akamjibu "Hata sijui, ila mimi binafsi nilileta lita 5 za maji, nikiwa na imani wengine mtaleta maziwa, kwahiyo hapata haribika kitu". Yule wa kwanza kuuliza swali akashtuka na kusema "Hata mimi nilileta lita 5 za maji nikijua nyie wengine mtaleta maziwa". Hapo hapo mwakilishi watatu bila kujua wenzake wanajadiliana nini, akasema anaomba radhi maana alileta maji badala ya maziwa.

Wanakijiji wote wa kijiji cha JamiiForums walipeleka lita za maji badala ya maziwa.

***** ***** ***** ***** *****

Guys, always play your part. Fanya kilichosahihi hata kama hakuna anayekuona. Do for love, not for fame.

Kuna muda unaweza fanya kitu kisicho kizuri kwa mwingine, ila akafurahia badala ya kuchukia, maana wapo wanaojua kuridhika kwa kila hali.


Leo mzee wakijiji sina maneno mengi, ila naomba niwaache na quotation moja ambayo ningependa ikae akilini kwa kila mwanakijiji wa hiki kijiji chetu :

"INTENTION MEANS NOTHING, IMPACT IS EVERYTHING"

Chochote unachofanya iwe kwa nia njema au mbaya, matokeo yake ndio yatajadiliwa sana na kukumbukwa.

Do what is right, even if no one watching.

Regards.

Analyse

Mzee wa Kijiji.
 
Do for love. Not for fame
images%20(13).jpg
 
Back
Top Bottom