King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 51,638
- 68,576
Mademu siku hizi wana wanaume pembeni wengine ndio maana watoto tunabambikiwa kumbe wa mwanaume mwingine
Hivi kule Maternity Ward, huwa hakuna uwezekano wa watoto kukosewa na kupewa mama mwingine?...najua huwa kuna alama wanafungwa watoto mikononi
Kongosho inabidi tukapime. Pamoja na kuwa ulibeba ile mimba kwa miezi nane nina wasiwasi kama mtoto ni wako.ndio wanamme wachangamke sasa.
Haya mambo ya kila mita tano kuna bango la 'mganga toka Sumbawanga na naijeria, anaongeza nguvu'
ila hii sio 'random sampling', hawa ni wale walioenda kupima. Na hadi kufikia point kupima uwezekano wa kuwa kulikuwa na doubts upo.
Ingawa si wote, huu ni ushahidi kuwa ufuska kwenye ndoa umezidi. Ni ushahidi wa mmomonyoko wa maadili. Kwenye mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Dodoma, Kagera, Lindi, Mtwara na Zanzibar sijui hali inatisha kiasi gani? Tunajenga taifa la wanaharamu siyo? Nashukuru Mungu watoto wangu wote hufanana nami. Isitoshe mambo ya kuzaa nshamalizana nayo.
Kongosho inabidi tukapime. Pamoja na kuwa ulibeba ile mimba kwa miezi nane nina wasiwasi kama mtoto ni wako.
Nina wasiwasi wewe ni surrogate mother. Akyanani tena.
Bila shaka utakuwa mpare wewe. wale hawabahatishiWengine huwa hatuhitaji hiyo kitu kwa sababu tukifyatua
watoto utafikiri tuliingizwa kwenye fotocopy machine yaani
Kwa mama anachukua rangi tu lakini vingine vyote ni mimi
mwenyewe.
Mwanangu Kongosho ingawa una tabia chafu ya kuchakachua watoto nimekupata. Kwangu sina shaka na wanangu kwa vile wamezaliwa Ulaya. Niliwazalia kisiwani ambapo nashukuru Mungu hapakuwapo na waswahili toka Bongo au karibu na Bongo. Iisitoshe bi mkubwa wangu si kiruka wala mtu wa kutishwa na mapenzi ya wizi. Hivyo sina shaka. Nami ninao sita.
Ingawa si wote, huu ni ushahidi kuwa ufuska kwenye ndoa umezidi. Ni ushahidi wa mmomonyoko wa maadili. Kwenye mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Dodoma, Kagera, Lindi, Mtwara na Zanzibar sijui hali inatisha kiasi gani? Tunajenga taifa la wanaharamu siyo? Nashukuru Mungu watoto wangu wote hufanana nami. Isitoshe mambo ya kuzaa nshamalizana nayo.
Ila mwanangu Kongosho angalia miwaya. Inaweza kukukumba hata kabla hujazeeka ukafa kwa majuto. Hata ukizidaka nyingi kiasi gani hutazimaliza na tamaa haitaisha. Dawa ya kumaliza tamaa ni kuachana nayo na kutulia kwa mmoja. Nadhani kimeeeleweka. Ila kama unaona hilo la kugawa kama una ugomvi nayo ni deal go ahead and perish. Amen!
Asilimia 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao. Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.
Takwimu hizo za kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, zilionyesha kuwa katika kesi 50 za waliokwenda kupima, matokeo yalionyesha kuwa ni wazazi halisi wa watoto wao. Hata hivyo, idadi hiyo inayoonyesha kuwa kinababa siyo wazazi halisi wa watoto, imeshuka ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2008/2009 ambazo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu waliochukua vipimo hivyo wamebainika kuwa si wazazi halisi wa watoto hao.
Mkemia na Mtambuzi wa Vinasaba vya Makosa ya Jinai, Gloria Machuve alisema jana kuwa ni vyema ikitambulika kwamba takwimu hizo zinatokana na watu waliokwenda kupima baada ya kutokea migogoro ya kimapenzi na siyo takwimu iliyochukuliwa kutoka kwa Watanzania wote. "Hatusemi kuwa sasa wanaume wote Tanzania wanalea watoto ambao si wa kwao. Hizi ni takwimu za waliokuja kupima; yaani wale wenye matatizo," alisema.
Machuve alisema katika maabara hiyo, kesi nyingi zinazoonyesha kuwa watoto hao si halali, zimetokana na uhusiano wa ziada au usio rasmi baina ya wenza. "Kwa mfano, mwanamume ana mwanamke wa nje ya ndoa au mwenye uhusiano usio rasmi, halafu mwanamke huyo anadai mtoto ni wa huyo mwanamume, mara nyingi matokeo huwa si mazuri," alisema Machuve.
Aidha, Machuve alisema takwimu za kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 zinaonyesha kuwa tabia ya upimaji imeongezeka miongoni mwa Watanzania. Alisema mwaka 2005/2006, kesi za upimaji wa vinasaba zilikuwa 96 na mwaka 2008/2009 kesi hizo zilikuwa 113 wakati mwaka 2009/2010, kesi za waliokwenda kupima zilifikia 125.
Alisema watu wengi wanaojitokeza kupima katika miaka ya karibuni wanataka kufahamu uhalali wa watoto wao ili wawajibike kuwalea kihalali.
Ni wale wanaofanyiwa utafiti na mkemia mkuu wa Serikali - Habari - mwananchi.co.tz