DNA: Nusu ya watoto ni wa kusingiziwa

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,303
damu_safi.jpg

Asilimia 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao. Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.

Takwimu hizo za kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, zilionyesha kuwa katika kesi 50 za waliokwenda kupima, matokeo yalionyesha kuwa ni wazazi halisi wa watoto wao. Hata hivyo, idadi hiyo inayoonyesha kuwa kinababa siyo wazazi halisi wa watoto, imeshuka ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2008/2009 ambazo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu waliochukua vipimo hivyo wamebainika kuwa si wazazi halisi wa watoto hao.

Mkemia na Mtambuzi wa Vinasaba vya Makosa ya Jinai, Gloria Machuve alisema jana kuwa ni vyema ikitambulika kwamba takwimu hizo zinatokana na watu waliokwenda kupima baada ya kutokea migogoro ya kimapenzi na siyo takwimu iliyochukuliwa kutoka kwa Watanzania wote. “Hatusemi kuwa sasa wanaume wote Tanzania wanalea watoto ambao si wa kwao. Hizi ni takwimu za waliokuja kupima; yaani wale wenye matatizo,” alisema.

Machuve alisema katika maabara hiyo, kesi nyingi zinazoonyesha kuwa watoto hao si halali, zimetokana na uhusiano wa ziada au usio rasmi baina ya wenza. “Kwa mfano, mwanamume ana mwanamke wa nje ya ndoa au mwenye uhusiano usio rasmi, halafu mwanamke huyo anadai mtoto ni wa huyo mwanamume, mara nyingi matokeo huwa si mazuri,” alisema Machuve.

Aidha, Machuve alisema takwimu za kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 zinaonyesha kuwa tabia ya upimaji imeongezeka miongoni mwa Watanzania. Alisema mwaka 2005/2006, kesi za upimaji wa vinasaba zilikuwa 96 na mwaka 2008/2009 kesi hizo zilikuwa 113 wakati mwaka 2009/2010, kesi za waliokwenda kupima zilifikia 125.
Alisema watu wengi wanaojitokeza kupima katika miaka ya karibuni wanataka kufahamu uhalali wa watoto wao ili wawajibike kuwalea kihalali.

Ni wale wanaofanyiwa utafiti na mkemia mkuu wa Serikali - Habari - mwananchi.co.tz
 
kajipime wewe na baba yako kwanza ndio uje watoto wako
 
Sasa mie nimeshasomesha wengine wamemaliza chuo kikuu nafanyaje niwakane? na kwa nini akina mama zetu mnatufanbyia hivi jamani!?
 
Hii ripoti nilishawahi kuisikiaga, lakini kutokana kiwango kikubwa cha udanganyifu kilichopo kwenye NDOA hiyo inawezekana. Kwani hata wanawake walio kwenye NDOA ukiwatongoza hawakatai. Sijui kwasababu hawapati DOZI inayotosheleza, maana na wao binadamu tusiwalaumu tu. Ila jamani wenzao tunachoka saana kutokana na matatizo ya maisha, lakini woa wanajijali wao tu. Maana kiiukweli wanaume wengi hawaendi zaidi ya raundi moja ya heshima tu, wakati wenzetu wao wako fiti ile kinoma. Bahati mbaya sana gemu lenyewe kwetu sisi linahusisha brain 100%. Sasa ukichanganya na mahangaiko ya dunia, du, brain inakua overloaded.

Sasa hakuna jema, ukiwa huna hela bado anatafutwa mwenye hela, ukiwa na hela lakini unachoka katika kutafuta hiyo hela, anasajiliwa house boy au dereva anae peleka watoto shule.

Katika hali hiyo ndio naweza kukubali kua 50% or more, wamebugi meen.

Lakini, je kama mkemia mkuu amekosea, just human or machine error? Sisi tunakua na uhakika gani as they say in court, beyond reasonable doubt?
 
Hivi kule Maternity Ward, huwa hakuna uwezekano wa watoto kukosewa na kupewa mama mwingine?...najua huwa kuna alama wanafungwa watoto mikononi

Hiyo ipo sana ndugu yangu, tena wengine naskia wanacheza dili na wakunga ili wapate watoto wa jinsia wanayotaka wao ,anaweza akajifungua wa kike akapewa wa kiume kwa kukusudia
 
Inatishia kitu gani hiyo nivea?

hivi unajua kuwa 80%ya wazee wetu waliokwenda kupigana vita ya ed amin dada waliporudi walikuta wake zao wana watoto?na walinyamaza kimya ,sasa basi kama wewe ni wa enzi hizo jinyamazie kimya na kama baba yako alikwenda.asilimia kubwa sio baba zetu kabisa ,sasa basi usianzie mzigo mbali wewe kwanza anza kijipim akwa mama yako kweli wewe ni mtoto halali wa baba yako?then njoo upime wanao lasivyo nyamaza kimya!!na tena itakuta baba uako ni **** kapuku maskini mama yako akaona huyu ngoja nimshikilie hapa ili apate elimu umeipata sasa unachokonoa inawezekana kabisa ungeishia la saba wewe funga domo hilo.
kwa hili ndipo tumewaweza wanaume kwa kweli
 
Hiyo ipo sana ndugu yangu, tena wengine naskia wanacheza dili na wakunga ili wapate watoto wa jinsia wanayotaka wao ,anaweza akajifungua wa kike akapewa wa kiume kwa kukusudia
babab v unafikiri wale watoto wote ni wako??na wewe unadhani ni mtoto halali wa baba yako ??haya mambo yaacheni wanaume mtalia kama mbwa huko njiani wachaneni we songesha maisha yaende ilhali hakuna aliyekuja dai mtoto we lea tu atakufaa mbeleni
 
Last edited by a moderator:
hivi unajua kuwa 80%ya wazee wetu waliokwenda kupigana vita ya ed amin dada waliporudi walikuta wake zao wana watoto?na walinyamaza kimya ,sasa basi kama wewe ni wa enzi hizo jinyamazie kimya na kama baba yako alikwenda.asilimia kubwa sio baba zetu kabisa ,sasa basi usianzie mzigo mbali wewe kwanza anza kijipim akwa mama yako kweli wewe ni mtoto halali wa baba yako?then njoo upime wanao lasivyo nyamaza kimya!!na tena itakuta baba uako ni **** kapuku maskini mama yako akaona huyu ngoja nimshikilie hapa ili apate elimu umeipata sasa unachokonoa inawezekana kabisa ungeishia la saba wewe funga domo hilo.
kwa hili ndipo tumewaweza wanaume kwa kweli

Uzuri baba yangu hakwenda...halafu tatizo sio la mimi na baba yangu...ni la mimi na mwanangu. Mi naangalia kiroho zaidi,lol!
 
kuthibitisha ukweli wa vipimo vya DNA, we pima mama na mtoto wake bado havitakubaliana pia. Hii DNA ni DuNiA au?
 
kuthibitisha ukweli wa vipimo vya DNA, we pima mama na mtoto wake bado havitakubaliana pia. Hii DNA ni DuNiA au?
Huenda uzembe wa manesi unaweza kusababisha
kubadilisha watoto wanapokuwa Hospitali. Kama wa
kichwa anakosewa na kupasuliwa mguu watashindwa
kukosea na kubadilisha watoto?

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom