DNA ina mapungufu gani ? Kwanini isiamue kesi za ubakaji+

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,573
Nimekua mfuatiliaji sana wa kesi mbalimbali na kati ya kesi hizo ni za ubakaji. Nilichokigundua ni kua hakuna kesi rahisi kutengeneza kama ubakaji.


imeshughudia kesi nyingi ambazo zinaonekana kabisa kusukwa hasa kwa kuwatumia wanafunzi. Moja ya kesi ni kuwa kijana alituhumiwa kutembea na mwanafunzi katika mahojiano na wakili. Yule mwanafunzi akaulizwa huyo kijana ndio aliyemtoa bikra ? ? Wakili wa upande wa pili akazuia swali lisijibiwa ila mwanafunzi akajibu hapana. It means kuna walaji wengine.
Wakili akaomba kitumike kipimo cha DNA kubaini kama alihusika,, wakili wa utetezi akasema kwa kua binti hakupata ujauzito hakuna haja.

Siku ya hukumu kijana akahukumiwamiaka 30 jela, cha ajabu binti ndo alizimia badala ya yule kijana. Baada ya kufuatilia ikagundukika wazazi wa binti walikua na familia ya kijana walikua na mgogoro.
Baada ya kuzinduka alipoulizqa kwann alipata mshtuko wakati ndo alitendwa akajib hakujua kama kijana angehukumiwa miaka 30 jela.

Baada ya muda ikagundulika kijana hakua na mahusiano na na binti(mwanafunzi) bali dada yake ambaye alishamaliza chuo na ilishindikana kuoana kutokana na tofauti za kidini ambapo wazazi wa binti walimshinikiza kijana abadili dini. Iliposhindikana wakabwagana. Akaona mwanamke mwingine.
 
Kwa sasa haya mambo yanawezekana, kupitia DNA unaweza kujua kama jamaa alimwingilia au lah, labda pengine jamaa hakuwa na uelewa au wakili wake naye kanjanja, ila angeomba vipimo na majibu ya DNA kudhibitisha, na hilo lingethibitika, maana huwez sema uchunguzi wa kesi ya ubakaji umekamilika, kama hakuna forensic investigations zinazomhusisha mtuhumiwa na kitendo alichofanya.
 
Tatizo ni namna ya kupata sample toka kwa binti, hapo ndio pagumu na sijui kwa nini jeshi la polisi na serikali kwa ujumla haufanyi jitihada kuielimisha jamii namna ya kutunza ushahidi kwa kesi za ubakaji.

Unakuta mtu anasema amebakwa wiki moja imeishapita, hapo kuja kupata uthibitisho kwa kutumia DNA ni ngumu sana mtu ameishaoga, kabadili nguo, kachana nywele nk halafu ndio anaenda polisi kushtaki.

Ifikie mahali hizi kesi zisiwe zinachukuliwa maamuzi haraka haraka kwa ushahidi wa kusikiliza pekee, kwa sababu sasa zimekuwa nyingi kila siku mpaka inatia shaka kuwa huenda nyingine ni za uongo.
 
Tatizo Ni Elimu Elimu Pia Kipimo Kinaweza Kikawa Kinafanyika Sehemu Chache Kwa Jinsi Inavyoonyesha Tupo Nyuma Kimaendeleo Ya Sayansi Na Teknolojia
 
tutoke nje ya DNA kidogo, baada ya ukweli kujulikana kwamba ulikuni uhasamawa kifamilia kijana alifutiwa ukumu yake ya miaka 30 jela au ndo ananyea ndoo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom