DMV USA: Kumuona Kikwete ni $100 kumpongeza kwa kuzalisha 3000mega watts za umeme

subiri bwana wako mbowe aje akuambie. maana umeshikiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na akili zako.

Wamaechanganyikiwa hao, huo umeme upo wapi?

Kama Dar kwenyewe umeme ni mgao hizo m zipo wapi?

Mabox yamewazidi ok uraia pacha wamefikia wapi?
 
kwani huko siju DMV sijui,ndio eneo ambalo hawa wamatumbi wenzetu toka tz wanapatikana kwa wingi zaidi?.kwanini kila siku ni DMV na isiwe portola valley california, piney point village texas, south beach florida, bloomfield hills michigan au clyde hill washington?.nimeuliza tu wakuu

Hapo DC ndio penye makao makuu ya World Bank na IMF. Kipindi hichi cha General Assembly Vingozi wengi omba omba lazima wapite huko.
 
Tanzania nakupena sana ila Tanganyika ni zaidi yako.JK kaenda kutiletea neema wananzengo eko baba Mwanahasha weye.
 
Akiingia madarakani 2005 idadi ya Watanzania ilikuwa chini ya milioni 40 na sasa inakaribia milioni 50, tulikuwa na ukame lakini sasa mvua ni za kumwaga sana sana tunahangaika tu na mafuriko, safari za kutoka mjini hadi Airport ilikuwa inachukua saa moja lakini leo hata ukitaka kuuchapa usingizi rukhsa kwani unao muda wa kutosha njiani, wana Diaspora walikuwa wanakaribishwa lakini leo ndio wanakaribisha, bei ya kilo ya sukari...duh, orodha ndefu kweli kweli! ni kweli anastahili pongezi nyingi tu. Asanteni DMV mmefanya la maana sana.
 
Tuende mbele turudi nyuma....1st July 2013 hadi 30th June 2014, JK kaenda mara ngapi US?? Tuwe realistic, binafsi naona kazidi sasa. Nafikiri hata wenyewe US wamemchoka sasa!!
 
- Duh sasa aliyepanga kumuona kwa kulipishana si waliomualika sasa kosa la Rais lipo wapi? Yaani mliambiwa upinzani ni kupinga pinga tu sasa kwa njia hii ndio mtashika dola? hahahahahaha

Le Mutuz

$100 kwa show ya JK kuimba Live band au atatumia Play Back? Huyu Rais yupo cheap sana...hajitambui
 
This is an insult to our Presidency ..nani kuruhusu hili ..yaani watu wanalipa dola ticketb100 kumuona Rais wa Nchi Kwani Kawa yeye Ndio DIAMOND au KANDA BONGO MAN..those days ..?
Hata Kama ilikuwa lengo ni fundraising si wangeandaa tu hicho chakula ...waalikwa watatoa pledge !!! Na Sasa fundraising ya watu wa box ...Wakati anaweza kuongea na Kina CarlMasters wakamuandalia fundraising ya watu wasiozidi 20 ..wafanyabiashara na wanasiasa ..wakaongea biashara na sio kuchangisha ..NGuo Za MITUMBA ambazo ni kazi zinafanywa na MAPADRI na wachungaji wakija Huko ...
Kama watu walishindwa kuchanga hizo dola 100 ..ili wa tume mjumbee wao wa katiba ...na hata aje na watu hata watano tu wa kufanya lobbying ili Uraia PACHA upite ...inawasaidia nini Leo Kulipa dola 100 kuhuddhuria show ya JK?
Kila mtu anajuwa namna diaspora walivoshindwa kabisa kutoa Mchango wa maana kwenye katiba ..kisheria na kubakia kupiga kelele mitandaoni..na kungoja show Za wasanii wa Tanzania ili walipe hizo dola waingie
 
Wana DMV, jitokezeni na mabango kupinga misafari isiyokuwa na tija inayofanywa na Mh JK. Kama hao wachache wenye kuona umuhimu wa kumpongeza JK, wameshindwa nini kwenda magogoni na kufanya hivyo? Walipa kodi tujiandae na mabango hapo Mariot, kupinga huu ufujaji wa pesa za walala hoi
 
nasikitika sana kumuona Raisi wangu nachangia pesa? tena dola $100? hamwezi kuwa serious so hiyo $100 ikitolewa kuna chakuna na vinywaji? au mnampa Rais Kikwete au waandaaji? ACHENI WIZI DMV
 
Nyie DMV mna akili za kitoto Sana, ninachoona Mimi hapa ni PURE KUJIPENDEKEZA kwa ajili ya maslahi binafsi na ubinafsi.

Ni kweli kwamba JK amejitahidi kusambaza umeme vijijini, kwa kiasi kikubwa sana. Hii ni kutokana na shilingi 50 ninayokatwa directly nikinunua lita ya mafuta, petrol or diesel, amefanywa vizuri because of my money.

Ni kweli kaongeza hizo MEGAWATTS, lakini ni kwa kupitia kampuni za kitapeli kama Symbion yenu, IPTL, Songas, Aggreko na matapeli wengine ambao wanazalisha umeme ghali mno kwa mlalahoi Mimi kumudu.

Kweli JK amejitahidi kujenga barabara, ingawa sehemu kubwa alirithi miradi inayoendelea toka kwa Mkapa. Innovation ya barabara binafsi nampatia Mkapa kwa vile alifanya pale pagumu. Sasa tuangalie ubora wa barabara za Kikwete zilivyo. Wewe uko DMV unabeba box haujui kuwa kutoka eneo linaitwa Bwanga wilayani Chato hadi eneo linaitwa Kyamyorwa wilayani Muleba kuna kilomita 150 za lami ambazo sasa ni mashimo na mahandaki chini ya miaka mitatu toka mradi ukamilike. Barabara zinazojengwa sasa ni kumtafutia lawama raisi ajaye kuwa ndio amebomoa kilomita nyingi za rami kuliko raisi yoyote but kumbe ubora ni feki.

Kama unahusisha kila mafanikio na Dr Kikwete basi husisha pia kila matatizo na yeye. Mfano kwa sasa kuna zaidi ya 50% ya shule za msingi ziko mjini kabisa wanafunzi wanakaa chini sakafuni. Karibu dispensary zote na vituo vya afya havina dawa. Mitaani kwetu takataka zimerundikana hadi aibu. Vijijini wanafunzi wanasoma chini ya miti hakuna majengo ya madarasa
 
Natoa sahihisho. Sio wakazi wote wa DMV wamehusika katika mpango huu wa kumsherehekea Kikwete kwa dinner ya dollar mia moja. Mratibu wa mpango huu ni kijana anaitwa Peter Ligate yuko California akishirikiana na tawi la CCM katika eneo hili la DMV ( District of Columbia, Maryland and Virginia) Baadhi yetu tuko mbali sana na mipango hii.
 
Hii mipumbavu ya DMV inastahili kucharazwa mikwaju mattakoni.
Nyani,
With all due respect. Huu ni mpango wa maCCM ya DMV. Sisi wengine hatumo kabisa kaka. Usituhukumu sote and I am sure I am speaking for the majority. BTW it is good to see you. It has been a while.
 
Back
Top Bottom