Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Ni kama ndoto ya mchana tena ya kijinga lakini ni ndoto ya mtu wa kweli aliyoishi nayo tangu alipozaliwa mpaka sasa ana umri wa miaka 35.
Wakati binadamu wengine wakifikiri juu ya kubadili aina ya maisha ya binadamu kupitia vishikizi vya mitandao ya kijamii, Mrusi bilionea wa intaneti anafikiri tofauti. Yeye anataka kubadili mwisho wa maisha ya binadamu duniani kwa kuhuisha na kuhifadhi ubongo wa binadamu kwenye kompyuta.
"Ndani ya miaka 35 ijayo nitahakikisha tunaishi milele", ana ahidi Dmitry Itskov. Sauti yake laini inazungumza kwa kujiamini huku kijana huyu aliyeamua kuacha biashara zake na kujikita katika kuitekeleza ndoto yake anasema ameamua kujichimbia katika kisima cha kutoa mchango wa ubinadamu. "Nina uhakika 100% nitafanikiwa, vinginevyo basi nisingeianza shughuli hii". Ni mawazo yanayohitaji kuvuta pumzi kuu lakini je, yatafanikiwa? Swali hili hapendi kujiuliza kila mara Dmitry.
"Ikiwa hakutakuwa na teknolojia hiyo (immortality technology) nitakufa miaka 35 ijayo" ameapa Dmitry Itskov. Kifo hakizuiliki maana kwa kadri umri unavyokwenda seli za mwili hudhoofika hivyo mwili hupoteza kinga dhidi ya magonjwa hususani magonjwa ya pumu na moyo yanayoua 2/3 ya binadamu duniani.
Kwa hiyo Itskov ameamua kuwekeza sehemu ya mkate wake katika mpango wake imara wa kurefusha maisha. Anataka kuitumia sayansi tata kuzifungua siri za ubongo wa binadamu na baadaye kuziunganisha katika mfumo wa kompyuta ambapo ubongo utakuwa huru dhidi ya maradhi ya kibaiolojia.
Lakini je, jambo hili linawezekana kweli kwa sisi binadamu wote duniani ku upload bongo zetu na kuzihifadhi katika kompyuta nje ya teknolojia iliyozoeleka yaani sci-fi?
Mkurugenzi wa kituo cha Mpango wa Itskov 2045, Dr Randal Koene ambaye pia amewahi kufanya kazi kama profesa mtafiti katika chuo kikuu cha Boston katika kitengo cha kumbukumbu na ubongo aliyepuuza aina ya kila kicheko katika suala hili, amesema inawezekana Itskov amepoteza ufahamu wa hisia na kuuchanganya na ukweli.
"Ushahidi wote anaotuonyesha kwenye nadharia unawezekana, ni jambo gumu sana lakini linawezekana" Anaongeza, " mtu yeyote anayefikiri kwa namna yake ni mtu wa maono, siyo mwehu kwa kuwa tu anafikiri juu ya vitu ambavyo kwa sasa haviwezekani"
Majibu ya Dr.Randal yanatokana na ukweli kwamba sayansi bado haijajibu swali juu ya namna ubongo unavyofanya kazi. Ubongo wa binadamu umeumbwa na neurons zinazokaribia bilioni 86.
Naye Prof Rafael Yuste wa chuo kikuu cha Columbia ameongeza kuwa ugumu utakuwa katika kuunganisha taarifa zilizopita katika viungo vya mwili, kuzipeleka katika fikra, kumbukumbu na hisia. Macho ya wadadisi wa mambo ya kisayansi wanalitazama jambo hili kwa jicho pevu huku wakigawanyika katika maoni yao ikiwa inawezekana au la.
Nini maoni yako mwana JF?
SOURCE:The immortalist: Uploading the mind to a computer - BBC News