Dkt. Tulia: Hakuna namna ya kuzuia watu kuamini kuwa Bunge limemezwa na Dola, lakini Bunge linafanywa kazi kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,222
5,946


===========

Alichoongea Bungeni Tulia Ackson wakati akiomba kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la Tanzania
Jina langu naitwa Tulia Ackson, nami kama wagombea wengine nimekuja ili niombe ridhaa yenu waheshimiwa wabunge ili kuhahakisha taifa letu linapata maendeleo basi niwe nawaongoza halafuwote tunaenda kwa pamoja kama wabunge. Pengine kinachinitofautisha mimi na wagombea wengine ni kuwa mimi ni mbunge mwenzenu.

Waheshimiwa wabunge ninawaomba ridhaa hii nikiwa natambua kazi kubwa ya bunge lakini pia kazi kubwa ya hayo mamlaka ambayo kama mtanipa ridhaa hii basi nitakuwa nayo. Sasa kwa sababu nimepewa dakika 3 sisi kama wabunge kazi yetu kubwa ni kuisimamia na kuishauri Serikali kuhahakisha inapeleka maendeleo kwa wananchi.

Na kazi kubwa ya Spika ni kuliongoza bunge katika majukumu hayo ambayo bunge limepewa kikatiba kwa hiyo waheshimiwa wabunge mkinipa ridhaa ya kuwa Spika wa bunge hili nitaliongoza bunge hili kwa muktadha hiyo wa kuhahakisha wabunge mnapata fursa ya kuihoji Serikali kwa heshima na kwa busara na kwa kufuata kanuni zetu lakini pia waheshimiwa wabunge mtapata fursa ya kutumia haki yenu ya kuwawakilisha wananchi kwa kuleta hoja zenu mbele ya Serikali.

Ili Serikali iweze kuangalia vipaumbele inavyoweka lazima isikilize wananchi wanasema nini na ninyi ndio wawakilishi wao. Katika uwakilishi wenu huo basi mimi kazi yangu itakuwa ni kuwapa fursa ya kutoa hoja zenu ambazo zitakuwa zimetoka kwa wananchi. Kwa sababu bunge kimsingi ni daraja kati ya wananchi na Serikali na hapa tunaongozwa na Waziri Mkuu ambaye kimsingi ni metendaji wa shughuli za Serikali kwa humu Bungeni ambapo yeye hutaka kujua wananchi wanasema nini na yeye akishasikia anajua kwamba wabunge wameleta mawazo ya wananchi.

Maswali Aliyoulizwa na wabunge
Swali: Mrisho Gambo:- Kwa kuwa bunge hili lina wabunge wengi wa CCM na wananchi wanaamini kwamba ni rahisi kwa bunge kumezwa na Serikali na hivyo kushindwa kwa bunge kuisimamia na kuikosa serikali Je, Mheshimiwa Dkt. Tulia tukikuchagua kuwa Spika unatuhakikishiaje kulinda heshima na hadhi ya Bunge ndani na nje ya bunge hili?

Jibu: Dkt. Tulia Ackson:- Nami nilijibu swali hili kwa muktadha wa majukumu yetu sisi kama wabunge kama muhilmili ambao umepewa kazi kikatiba wa kuisimamia Serikali wa kuishauri Serikali, haijalishi kuwa yeye ni mbunge wa chama cha Mapinduzi au ni mbunge wa Chama cha Upinzani anapoleta hoja humu Bungeni yeye ni mwakilishi wa wawananchi sasa kwenye hoja kwamba bunge kwa sababau lina wabunge wengi wa CCM linaweza kuimeza Serikali huo uwezekano haupo.

Kwa sababu Serikali haiwezi kulimeza Bunge na au Bunge kuimeza Serikali kwa sababu katiba yetu imeweka majukumu tofauti Bunge kazi yake ni kuishauri na kuisimamia Serikali kuhakikisha serikali je utendaji wake unaleta tija kwa wananchi au lana Serikali kazi yake ni utendaji. Ndio maana mwenyekiti wakati anafungua kikao alieleza namna ambayo serikali inapeleka maendeleo katika majimbo yote.

Kwa hivyo unavyopeleka hayo maendeleo huko kwa wananchi na wanacnhi watapata kusikia namna ambavyo serikali imefanya kazi kubwa huko kwenye majimbo na serikali itasikia namna ambavyo pamoja na kazi iliyofanywa na serikali ila changamoto zipo na watasikia wabunge wakileta hoja zao bungeni. Hivyo sababu kuwa kuna wabunge wengi wa CCM maana kila mbunge amechaguliwa kwenye jimbo lake kwa uwezo wake wa kuwaongoza wananchi waliompa ridhaa hiyo.

Swali: Aidan:- Tulia amesema kazi ya Bunge ni kuisimamia na kuishauri serikali, Sura iliyopo huko nje pamoja na kwamba serikali yetu inaongozwa na mihimili 3 katika kupeleka maendeleo kwa wananchi. Kushirikiana na mihimili mitatu kepeleka maendeleo kwa wananchi sio jambo baya, jambo baya linakuja pale ambapo mhimili mmoja unapotaka kuingilia shughuli za mhimili mwingine. Tunataka kujua umejipangaje katika kuondoa sintofahamu kwa watanzania ya kuweza kulinda hadhi na heshima ya bunge.

Jibe: Tulia Ackson:- Katika miaka 6 ambayo mimi nimekuwa naibu spika na huu ni wa saba ambapo mimi nagombea kuwa Spika hakuna wakati wowote ambapo Serikali ililiingilia bunge au bunge kuingilia serikali. Na mimi kama kama nilivyoeleza hapo awali mkinipa ridhaa bunge hili litaendeshw akwa mujibu wa katiba na kanuni tulizojiwekea. Kama nilivyoeleza sisi ni wawakilishi wa wannchi na bunge ndio daraja kati yetu na Serikali wakati mwingine watu huwa wanafikiri daraja hili linaweza kukaa kwa namna fulani hivi gari lisipite aaa hapana kazi ya daraja ni kuvusha vitu viende upande wa pili, kuchukua hoja za wananchi kupeleka serikalini.

Lakini pia bunge linao uwezo wa kuiwajibisha serikali kama kuna mambo yatakuwa sivyo hivyo wsiwe na wasiwasi na kwa kuwa sisi ndio wawakili wa wananchi na wananchi ndio wametuleta humu basi tutakwenda kupeleka hoja zao.
 
5678901.jpg
 
"Wewe wabane huko ndani, wakitoka nje nitawashughulikia" kwa sauti ya JPM akimuagiza JYN.
 
Nje na kufanya kazi kwa mujibu wa katiba, sheria na kanuni, kuna njia gani nyingine ya kulifanya bunge "lisimezwe" na serikali ?

Maana naona tunalalamika tu kama kawaida yetu.

Mkuu GUSSIE njoo uwaone watanzania wenzetu wanalalamika tena huku.
 
Eti Tanzania tuna Bunge? FCXEWASYYY!!! 😴🥳 Huu uzwazwa sijui utaisha lini. Kodi za walalahoi zinaliwa na watu asio na mchango kwa taifa
 
Eti Tanzania tuna Bunge!!?? FCXEWASYYY!!! 😴🥳 Huu uzwazwa sijui utaisha lini. Kodi za walalahoi zinaliwa na watu asio na mchango kwa taifa
Kwanza hoji zile zaka unapeleka kwa Mwingira
 
Basi hizo Katiba na Kanuni Hazifai.

Issue kubwa kuhusu Haki sio kwamba tu itendeke bali ionekane pia kwamba imetendeka.

Sasa kama kila mtu anaona kwamba imemezwa alafu yeye na wenzake pekee either wanaona haijamezwa au umezwaji huu ni sawa (basi watoe mambo ya mihimili ibaki miwili au mmoja) hakuna sababu ya kuendelea na maigizo kwa kutumia pesa zetu za Kodi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom