Dkt Tulia azungumzia tetesi za kugombea ubunge Mbeya, ‘Ni haki yangu’

MumbaZ

Senior Member
Jan 28, 2018
133
124
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amejibu tetesi zilizosambaa kuwa ana mpango wa kugombea ubunge katika jimbo mojawapo mkoani Mbeya.

Akizungumza na Dar24 ofisini kwake katika mahojiano maalum hivi karibuni, Dkt Tulia alisema kuwa yeye kama raia wa Tanzania ana haki yake kikatiba kugombea lakini bado hajaweka wazi eneo atakalogombea nafasi hiyo.

“Ni haki yangu ya kikatiba kugombea, lakini sijasema bado nitagombea wapi. Na nadhani wakati huo nitakapofanya maamuzi watu watayasikia kwa sababu huwa sio siri. Lakini kwa sasa hivi najaribu kufanya hizo kazi za kijamii lakini sio kwa lengo la kugombea hasa,” Dkt. Tulia aliiambia Dar24.

Alifafanua kuwa kama ni kugombea ubunge, ni jimbo moja linalotakiwa lakini kazi za kijamii anazofanya zinahusisha maeneo yote nchini.

Dkt. Tulia aliteuliwa kuwa Mbunge na baadaye kugombea nafasi ya Unaibu Spika wa Bunge nafasi ambayo alifanikiwa kuipata na anaitumikia hadi leo.
 
haki na mipaka yake usisahau hilo... hata kama una jua sheria...
 
Kwa jinsi hali ilivyo na matukio yanavyoenda naona kabisa huyu Mama ndiyo atasimamishwa na Sugu itakapofika 2020 na CHADEMA wakizubaa kuna hatari ya goli la mkono. Tuombe Uhai tu ili tuje kuyashuhudia
 
Huyo msugusugu hana sifa tena ya kugombea. Aliye mshauri kukata rufaa kamdanganya, ajiandae kuongezewa mvua nyingine kwa kushindwa rufaa. Mark my words.
 
Kwani kunampango wa kumfanya kuwa sabwufa kamili?......vipi jamaa yetu wa Hollywood?
 
Huyo msugusugu hana sifa tena ya kugombea. Aliye mshauri kukata rufaa kamdanganya, ajiandae kuongezewa mvua nyingine kwa kushindwa rufaa. Mark my words.
Kwa hilo lihukumu la kijinga hakuna jaji anayeweza kukubaliana nalo, wala hatuna haja ya "ku mark your words"!
 
Huyo msugusugu hana sifa tena ya kugombea. Aliye mshauri kukata rufaa kamdanganya, ajiandae kuongezewa mvua nyingine kwa kushindwa rufaa. Mark my words.
Nyie bush lawyers mnashida sana. Lini uliwahi kusikia mtu anaongezewa adhabu akishindwa rufaa?
 
Unamshangaa Jesca wakati baba yake mnauliza PHD yake kilasiku?
PHD feki na ya Jesca pia ni ya kuunga kwa gundi.
 
Back
Top Bottom