Dkt Tulia azungumzia tetesi za kugombea ubunge Mbeya, ‘Ni haki yangu’ | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dkt Tulia azungumzia tetesi za kugombea ubunge Mbeya, ‘Ni haki yangu’

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MumbaZ, Feb 21, 2018.

 1. M

  MumbaZ Senior Member

  #1
  Feb 21, 2018
  Joined: Jan 28, 2018
  Messages: 129
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amejibu tetesi zilizosambaa kuwa ana mpango wa kugombea ubunge katika jimbo mojawapo mkoani Mbeya.  Akizungumza na Dar24 ofisini kwake katika mahojiano maalum hivi karibuni, Dkt Tulia alisema kuwa yeye kama raia wa Tanzania ana haki yake kikatiba kugombea lakini bado hajaweka wazi eneo atakalogombea nafasi hiyo.

  “Ni haki yangu ya kikatiba kugombea, lakini sijasema bado nitagombea wapi. Na nadhani wakati huo nitakapofanya maamuzi watu watayasikia kwa sababu huwa sio siri. Lakini kwa sasa hivi najaribu kufanya hizo kazi za kijamii lakini sio kwa lengo la kugombea hasa,” Dkt. Tulia aliiambia Dar24.

  Alifafanua kuwa kama ni kugombea ubunge, ni jimbo moja linalotakiwa lakini kazi za kijamii anazofanya zinahusisha maeneo yote nchini.

  Dkt. Tulia aliteuliwa kuwa Mbunge na baadaye kugombea nafasi ya Unaibu Spika wa Bunge nafasi ambayo alifanikiwa kuipata na anaitumikia hadi leo.
   
 2. L

  Libertatem Pugnator Senior Member

  #21
  Mar 2, 2018
  Joined: Aug 24, 2017
  Messages: 168
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Hebu niambie kesi yoyote unayoijua kwamba kwenye appeal adhabu ya subordinate court huwa inaongezwa na appellate court pindi appellant anaposhindwa kwenye hiyo appeal. Just one case please ili nijifunze kutoka kwako
   
 3. jaji mfawidhi

  jaji mfawidhi JF-Expert Member

  #22
  Mar 2, 2018
  Joined: Feb 20, 2016
  Messages: 3,781
  Likes Received: 2,865
  Trophy Points: 280
  eti tulia mlokole wakati akishirikiana na makala wameandika hukumu ya ovyo tangu nani avunje ungo
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...