Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia atema cheche Mbeya Mjini, awajibu Lissu na Sugu kuhusu maendeleo ya vitu watu wafurika mkutano wake

Mkuu kwenye maendeleo zinatumika zaidi dhana mbili; Rostow's Stages of Development na Marxist Stages of Development kutegemea una mrengo gani kisiasa. Wote wanakubaliana kwamba Maendeleo ya Watu ndio hatua ya juu kabisa (High Mass Consumption kwa Rostow) na (Communism kwa Marxism) ya maendeleo ya mwanadamu.

Kama ninyi na Lissu wenu mnaweza kutuaminisha tofauti kwamba unaweza kusafiri kwa haraka kati ya Mwanza na Dar (maendeleo ya watu) bila ndege au SGR au watu kuwa na umeme wa uhakika (maendeleo ya watu) bila kuzalisha umeme wa kutosha na wa uhakika inawezekana, mimi nitaunga mkono hoja.
Mkuu umeshirikisha ubongo kweli?
 
Ni ujinga kudhani una2eza kuendelea bila kuwa na miundo mbinu. Kama ni hivyo mchagueni Cheyo wa UDP. Yeye alikuwa anawajaza Mapesa mifukoni.

Hawa wanasiasa wasifikiri kila mtu ni mpumbavu kiasi hicho kwamba, Haulimi, hauna uzalishaji unaowezeshwa na miundombinu halafu una hela, kwahiyo serkali iwe inawapelekea watu hela majumbani.

Huku wanasema hakuna ajira, ajira bila miundo mbinu utaipata wapi?

Yaani wote tuwe watumishi wa Umma, inawezekana?

Huku wanasema Kaua sector binafsi.

Wanadhani wote tunaelewa inaposemwa miundombinu inamaanisha reli, barabara na viwanja tu. SIO

Siko ssm yenu, sitapiga kura, kadi ipo, ILA Upinzani unaonyesha haujakomaa kupewa nchi.
Mkuu unaelewa kweli hoja ya wapinzani wanaposema maendeleo ya watu na siyo vitu? So maelezo yako hapo juu ndiyo wew umeelewa hivyo?
Kweli Tanzania wajinga ni wengi
 
Kwahiyo umeme wanatumia mbwa? Ndege wanapanda wanyama? Barabara wanapita mbuzi? Akili za wapi hizi unatumia!?
Kabla ya hizi ndege zenu tulikua tunapanda FastJet kwa bei pouwa tu! Tatizo siyo kununua ndege tu, lakini Kwanini serikali ijiingize kwenye biashara? Na kwenye ushindani sokoni unauwa wapinzani (kibiashara) kama hawa kina fastjet, ili utawale soko??! Mbona serikali haina basi hata moja, lakini tunasafiri kila leo?
 
Hapo ndio mnapofeli,sasa sura sijui umbile lake linahusiana vipi na nafasi anayogombea!? kwamba sugu handsome? acheni ubaguzi wa kimaumbile kwani aliyekuumba wewe ndiye aliyemuumba yeye
tofauti wazazi tu.wabagueni kwenye hoja
Failure inputs zinaanzaga hivyo,hata huyo Mbunge Sugu hapendezewi na tabia hiyo ya kunyayapaa wanawake.
Hivi anadhani wanawake warembo ndio anataka tu wampigie kura Sugu tu?Hajui kwa kauli za kijinga kama hizo zinaweza zikaangusha hata tembo?
Ni bora huyo jamaa afute usemi wake.
 
Mkuu unaelewa kweli hoja ya wapinzani wanaposema maendeleo ya watu na siyo vitu? So maelezo yako hapo juu ndiyo wew umeelewa hivyo?
Kweli Tanzania wajinga ni wengi
Soma kitabu cha Mdee , angalau ujue maendeleo aliyopeleka Kawe.
Halafu uje u comment
 
Jana nimekutana na watu wanaimba tulia ni hatari kuliko virus vya corona😀😀😀😀😀at hafai kuwa kiongozi afu ni akina mama
 
Mbeya pagumu sana raia hawamtaki Tulia aka Betina hadi anaowapa rushwa wapiga debe wote wamevaa jezi zake lakini wanakwambia KULA kwa Tulia lakini KURA kwa sugu
 
Back
Top Bottom