Dkt. Tulia amjibu Mbunge aliyehoji kuhusu Uwanja wa Ndege Msalato. Asema Rais kashasema utajengwa

Naibu spika amesema kuwa "ujenzi wa uwanja wa ndege wa msalato utafanyika hata kama haupo kwenye bajeti maana rais ameshasema na neno lake ni sheria" mwisho wa nukuu.

Ole Sabaya alikuwa akitekeleza amri za bosi wake Hayati John Magufuli. Mfano Magufuli aliwataka watendaji wake wahakikishe mapato yanakusanywa kwa namna yoyote ikiwemo uporoji wa TRA, wapinzani wanahujumiwa kwa namna yoyote.

Nani alikuwa anamkosoa MAGUFULI? Mwanaccm yupi alipinga mawazo ya JPM? Acheni double standard. Kama mwanasheria anasema neno la rais ni sheria je SABAYA anakosa gani?
 
Dah! Maspika wetu hawa yaani

Hili swali ilitakiwa kabisa spika ndio aulize au kama mbunge akiuliza basi ilitakiwa spika amuunge mkono kuhitaji majibu kujua iwapo uwanja bajeti yake haijatengwa utajengwaje!

Angalia jibu lake lakini "Rais amesema Uwanja utajengwa, kwa hiyo kama upo au haupo kwenye Bajeti Rais kashasema, ndio Sheria hiyo"
Kwa hiyo mbunge hana haki kuuliza kwasababu Raid kasema?mini maana ya MIHIMILI.
TULIA UNAENDESHA BUNGE KWA MATAMKO YA RAIS,AKIJA RAIS MWINGINE NA TAMKO?

WABUNGE PIGENI KURA WAONDOKE HAO WENYE KINGA.HAWANA MSAADA KWENU
 
Yapo hivyo hivyo mkuu, nimeona video kwa Millard Ayo...
OK. nimeiona clip kwenye bandiko namba 43 hapo juu.
Naibu spika bado anaota yale ya mwendazake hadi anasahau hata taaluma yake. Ni sheria gani inayosema tamko la rais ni sheria?
Hawa watu wanataka kumpoteza rais Samia. Ni kweli kasema uwanja utajengwa lakini tamko hilo siyo sheria kama Naibu spika anavyojaribu kutuaminisha. Ni kweli rais anaweza kuhamisha fedha toka fungu moja kwenda jingine kujenga huo uwanja na baadae kuja bungeni kuomba supplementary budget. Maana yake nini; budget ni sheria na ndiyo maana inapitia bungeni. Kama Rais atafanya tofauti na budget, kwa manufaa ya uma, then lazima aje tena bungeni kuliomba bunge litengeneza sheria ya nyongeza ya budget - ndiyo hiyo supplementary budget.

Naibu spika kwa kuonnyesha kuwa rais ana uwezo wa kuskip mhimili ambao yeye anauongoza, ni udhaifu mkubwa.
Nadhani aliteleza maana namna alivyotamka maneno "ndiyo sheria" ni kama hakuwa na uhakika na alichotaka kutamka.
 


Katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, amesema Naibu Waziri hawezi kusema kitu tofauti na alichozungumza Rais.

Amesema hayo baada ya Mbunge Kunti Majala kuhoji ni lini Serikali itajenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato akisema haupo kwenye Bajeti ya 2021/22.

Dkt. Tulia ameeleza, "Rais amesema Uwanja utajengwa, kwa hiyo kama upo au haupo kwenye Bajeti Rais kashasema, ndio Sheria hiyo".

Spika mpumbavu kuwahi kutokea,vyeo vya kupeana matokeo yake ndiyo majibu haya.
 
Miradi mingi iliyoachwa na JPM haitaendelezwa kwa sababu uwezo wa kukusanya fedha wa serikali hii ni mdogo sana watakuja na visingizio kua haina tija tunaipiga chini ukweli ni kwamba hawana fedha
Ila mwendakuzimu alikopa sana pesa, bora Mungu aliingilia kati, tungekoma hakika
 
Naibu Spika yuko sahihi. Ilani ya CCM iliyopo inaelekeza utekelezaji wa miradi hadi 2025. Kama haipo bajeti ya mwaka huu itakuwepo hata mwakani.
 
Kwahio Bunge haliwezi kusema lolote hata kama kesho Rais akisema tuuze nchi yetu, tununue nyingine ?
 
Tuna shida kama taifa. Spika sio msemaji wa serikali! Ni msimamizi mkuu tu wa taratibu za shughuli na taratibu za Bunge. Aliyepaswa kutoa taaifa aliyotoa Spika ni Wazara husika!

Rais sio mpangaji wa bajeti japo ni mshawishi na mtoa dira wa mipango ya serikali. Kamwe hawezi kupanga matumizi bila idhini ya Bunge!

Taasisi zetu hazifanyi kazi ipasavyo. Turekebishe hayo kwa katiba mpya!
 
Msalato Airport inajengwa kwa mkopo kutoka AFDB ambao ulishapitishwa kitambo sana, kuna tatizo kubwa kwa hawa wawakilishi wa wananchi, kabla ya kuropoka bungeni wanatakiwa kufanya utafiti

Ni wazi pia Dkt. Tulia hana ufahamu wa kinachoendelea kwa namna alivyomjibu kiwepesi huyo mbunge
Hilo jibu ndio lilikuwa litolewe bungeni, kwani siri?
 
Miongoni mwa takataka za jalalani za mwendazake.wakati mawaziri wanasisitizwa watoe majibu sahihi kwa maswali ya Wabunge.anaijibia serikali majibu ya ovyo kama sura yake
 
Tulia ana uhakika akilamba viatu vizuri come 2025 anakuwa Spika, wana Sera yao ya 50 50, sasa hivi itakuwa full kumtetea Odo..
 
Back
Top Bottom