beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, amesema Naibu Waziri hawezi kusema kitu tofauti na alichozungumza Rais.
Amesema hayo baada ya Mbunge Kunti Majala kuhoji ni lini Serikali itajenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato akisema haupo kwenye Bajeti ya 2021/22.
Dkt. Tulia ameeleza, "Rais amesema Uwanja utajengwa, kwa hiyo kama upo au haupo kwenye Bajeti Rais kashasema, ndio Sheria hiyo".