Nikweli mtaalamu ana PHD anaacha kwenda kufanya kazi kwenye mashirika au compuni zingine zenye maishahara minono end ekwenye ubunge hauna kituuu!!.Nimemsikiliza akiongea anaonekana kuwaaminisha watu wabunge hawapati kingi kama wakurugenzi wengine kwenye mashirika ya umma.
Lakini anasahau kwa idadi ya wabunge mara hizo posho na mishahara bado hesabu inakuwa kubwa, amesema wabunge pamoja na waziri mkuu wanafika 395 ukipiga mara hizo figure utaona wanavyolifanya taifa kuzidi kuwa masikini.
Kigezo kingine alichotumia ku-justify hizo posho zao amesema hata wafanyakazi wengine wa umma wakisafiri hulipwa pesa za usafiri na gharama nyingine.
Lakini tunaona hawa wafanyakazi huwa wanacheleweshewa posho zao wakati mwingine hawapati mpaka wanafika vituo vyao vya kazi, na hata mishahara huchelewa, hili kwa wabunge haliwezi tokea.
Issue nyingine aliyozungumzia kuhusu wabunge 19 waliokuwa wa Chadema, anasema Chadema ndio wanatakiwa kumaliza taratibu zao ndani ya chama ndio bunge liwaondoe au lah.
Hapa Tulia anajua fika mtu akishaadhibiwa adhabu yake huanza kutekelezwa pale inapotolewa, sio mpaka atakapokata rufaa either akishinda ndio asiadhibiwe, au akishinda ndio aadhibiwe, na KM wa Chadema alishawaandikia barua kuwajulisha kuhusu hilo, lakini nashangaa bado wanakuwa wagumu kuelewa.
Sio kqweli kuna vivutio fulani na maruprupu kibao ndio yanayo mfanya wasomi wote kukimbilia huko na kuhonga na kila kitu.