Dkt. Tulia Ackson: Mshahara wa Mbunge ni Tsh milioni 4.6 na sio vinginevyo

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,224
6,468
Ktk kipidi cha ITV Dk 45, mambo yabwagwa hadharani.

Hivi punde akihojiwa ktk kipidi hicho, Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania Mheshimiwa Dr Tulia Ackson, amedai mshahara wa Mbunge ni milioni 4.6 tu. Anakatwa Kodi Tsh 1500,000 na kubakiwa na Tsh 3100,000.

Ameendelea kudai posho ya kikao ni Tsh 120,000. Pia Kuna posho ya kumlipa Dereva na Katibu wa Mbunge na posho ya mafuta. Pia Kuna mfuko wa Jimbo.

Watu wa nje ya Bunge wakipiga hesabu wanadai ni Tsh 11,0000,000 jambo ambalo sio kweli. Hizo hela zinapita kwa Mbunge japo zote sio zake.

Kwa kauli hii ya Naibu spika wa Bunge ni dhahiri kuwa wabunge wanakatwa Kodi tofauti na uvumi uliopo mtaani.
 
Nimemsikiliza akiongea anaonekana kuwaaminisha watu wabunge hawapati kingi kama wakurugenzi wengine kwenye mashirika ya umma.

Lakini anasahau kwa idadi ya wabunge mara hizo posho na mishahara bado hesabu inakuwa kubwa, amesema wabunge pamoja na waziri mkuu wanafika 395 ukipiga mara hizo figure utaona wanavyolifanya taifa kuzidi kuwa masikini.

Kigezo kingine alichotumia ku-justify hizo posho zao amesema hata wafanyakazi wengine wa umma wakisafiri hulipwa pesa za usafiri na gharama nyingine.

Lakini tunaona hawa wafanyakazi huwa wanacheleweshewa posho zao wakati mwingine hawapati mpaka wanafika vituo vyao vya kazi, na hata mishahara huchelewa, hili kwa wabunge haliwezi tokea.

Issue nyingine aliyozungumzia kuhusu wabunge 19 waliokuwa wa Chadema, anasema Chadema ndio wanatakiwa kumaliza taratibu zao ndani ya chama ndio bunge liwaondoe au lah.

Hapa Tulia anajua fika mtu akishaadhibiwa adhabu yake huanza kutekelezwa pale inapotolewa, sio mpaka atakapokata rufaa either akishinda ndio asiadhibiwe, au akishinda ndio aadhibiwe, na KM wa Chadema alishawaandikia barua kuwajulisha kuhusu hilo, lakini nashangaa bado wanakuwa wagumu kuelewa.
 
Nimemsikiliza akiongea anaonekana kuaminisha watu wabunge hawapati kingi kama wakurugenzi wengine kwenye mashirika ya umma.

Lakini anasahau kwa idadi ya wabunge mara hizo posho na mishahara bado hesabu inakuwa kubwa, amesema wabunge pamoja na waziri mkuu wanafika 395 ukipiga mara hizo figure utaona wanvyolifanya taifa kuwa masikini.

Kigezo kingine alichotumia ku-justify hizo posho zao amesema hata wafanyakazi wengine wa umma wakisafiri hulipwa pesa za usafiri na gharama nyingine, lakini tunaona hawa wafanyakazi huwa wanacheleweshewa posho zao wakati mwingine hawapati mpaka wanafika vituo vyao vya kazi, na hata mishahara huchelewa, hili kwa wabunge haliwezi tokea.
Kweli kabisa, ni Kama haridhiki na mshahara na posho zao akitaka ziongezwe.
 
Kwanini alipwe pesa za mfuko wa jimbo (za umma) ziwekwe kwenye akaunti ya mtu binafsi (mbunge mwenyewe). Kwanini mbunge amlipe katibu wake kwa kwa kutumia pesa za umma huku hiyo nafasi upatikanaji wake hauwi wa ushindani? na huyo dereva wa mbunge huwa anapatikana kwa mchakato upi wa ajira?
 
P

Wajuvi mje mtusaidie majibu
 
Majibu ni mazuri. Lakini yalipaswa yatolewe pale tuu hili suala lilipoibuliwa na mbunge wao. Kwa kuchelewa ndio kunafanya watu wasiwaamini.

Amandla...
 
Kwanini alipwe pesa za mfuko wa jimbo (za umma) ziwekwe kwenye akaunti ya mtu binafsi (mbunge mwenyewe). Kwanini mbunge amlipe katibu wake kwa kwa kutumia pesa za umma huku hiyo nafasi upatikanaji wake hauwi wa ushindani? na huyo dereva wa mbunge huwa anapatikana kwa mchakato upi wa ajira?
Corruption! Mimi simsikilizi mdomoni, kwani vinywa vyao hutoa uozo. Labda nitamuona mkweli akiongea kwa makalio.
 
Nimemsikiliza akiongea anaonekana kuwaaminisha watu wabunge hawapati kingi kama wakurugenzi wengine kwenye mashirika ya umma.

Lakini anasahau kwa idadi ya wabunge mara hizo posho na mishahara bado hesabu inakuwa kubwa, amesema wabunge pamoja na waziri mkuu wanafika 395 ukipiga mara hizo figure utaona wanavyolifanya taifa kuzidi kuwa masikini.

Kigezo kingine alichotumia ku-justify hizo posho zao amesema hata wafanyakazi wengine wa umma wakisafiri hulipwa pesa za usafiri na gharama nyingine.

Lakini tunaona hawa wafanyakazi huwa wanacheleweshewa posho zao wakati mwingine hawapati mpaka wanafika vituo vyao vya kazi, na hata mishahara huchelewa, hili kwa wabunge haliwezi tokea.

Issue nyingine aliyozungumzia kuhusu wabunge 19 waliokuwa wa Chadema, anasema Chadema ndio wanatakiwa kumaliza taratibu zao ndani ya chama ndio bunge liwaondoe au lah.

Hapa Tulia anajua fika mtu akishaadhibiwa adhabu yake huanza kutekelezwa pale inapotolewa, sio mpaka atakapokata rufaa either akishinda ndio asiadhibiwe, au akishinda ndio aadhibiwe, na KM wa Chadema alishawaandikia barua kuwajulisha kuhusu hilo, lakini nashangaa bado wanakuwa wagumu kuelewa.
Kwa kauli yake mbunge Jery slaa alisema kabisa kuwa wabunge hawalipi kodi kabisa .

Sasa huyu anataka kumdanganya nani ambaye atamuamini?
 
Back
Top Bottom