Dkt. Tulia Ackson: Ilani inasema barabara ya Tanzam upembuzi yakinifu umekamilika Serikali inasema utafanyika mwakani. Tuiamini CCM au Wizara?

Matapeli bana huwa wana tabia ya kujichanganya sana. Serikali ni matapeli, na ccm wazee wa ilani ya kurasa 300 nao ni matapeli. Sasa wameanza kushikana uchawi.
Barabara za Mbeya na hata Songwe zimo kwenye ilani kwa miaka zaidi ya 20 , lakini hakuna kinachofanywa.
Hivyo ilani ya CCM kwa kweli kwa mikoa hiyo kuhusu miundombinu ni upuuzi mtupu.
 
Thubutu aulize swali kama hili enzi za dhalimu!!! Hizi ni dalili tosha kwamba ndani ya maccm mama ana hali ngumu sana.
Acha uzwazwa wako na mepenzi ya kijinga.
Kwani hapo anaulizwa raisi au waziri?
Mbona mnakoswa hoja mnabaki kudandia mambo.

Mbona mambo hayo yamekuwa yakiulizwa hata kipindi yupo huyo unaemtuhumu
Maswali yamekuwa yakiulizwa na ndugai kwa mawaziri
Mbona hukusema kwa nini anauliza wakati yupo huyo magufuli?
 
Wabunge wa Mbeya /Songwe wakomalie hii miundo mbinu ya mikoa hii.
Ukitoka pale Igawa kuelekea Mbeya barabra ni mbaya mbaya mno, unaweza hata kupoteza rim ya gari na kuingia korongo(Igawa-Mbeya ni 100km na Mbeya-Tunduma ni ~100km)

Mkapa hakuwahi kukarabati
Kikwete hakuwahi kukarabati.
Mwendazake alikuwa busy na fly over ya Busisi kwenda kwao.

Ni wakati kudai barabara hii na nyingine Mkoani Mbeya /Songwe zijengwe, tumenyanyapaliwa mno.
Kuna ile barabara ya Katumba kwenda Mwakaleli kwenye chai na gesi toka uhuru haijawahi jengewa lami!! WAkati inaingizia nchi mabilioni ya pesa zikiwemo za kigeni

Wabunge wa Mbeya komaeni
 
Wabunge wa Mbeya na Songwe wasipokomaa sasaivi miundombinu ya ule Mkoa ndo inaenda kuwa mfu kabisa. Haiwezekani mikoa inayochangia kwa kiwango kikubwa uchumi wa Taifa hili kutokana na kuwa njia kuu ya mizigo kwenda nchi kama 5 alafu inakuwa na miundombinu mibovu kiasi kile.
Kuna ile ya Katumba kwenda Mwakaleli kwenye chai na gesi toka uhuru haijawahi jengewa lami!! WAkati inaingizia nchi mabilioni ya pesa zikiwemo za kigeni

Wabunge wa Mbeya komaeni
 
Kuna ile barabara ya Katumba kwenda Mwakaleli kwenye chai na gesi toka uhuru haijawahi jengewa lami!! WAkati inaingizia nchi mabilioni ya pesa zikiwemo za kigeni

Wabunge wa Mbeya komaeni
Mkuu tena ile barabara inaelekea kwtu kwenye bridi.
Inabidi sisi tulioenda shule kidogo tuanze civil action kwani serikali kupitia Tanzania Oxygen Ltd(TOL) wamevuna sana Gesi ya Carbon Dioxide kule Kyejo na hakuna mrahaba wowote kwa vijiji na hata barabara bado ni mbovu sana.
Mbunge wa eneo hili atake note kuwa kuomba barabara hii ni wajibu.

Mbaya zaidi Ilani zote za CCM zimeitaja hii barabara miaka yote ya uchaguzi, lakini ni uongo mtupu.
 
Mbunge wa Mbeya mjini Dr Tulia Ackson amesema kuna mkanganyiko mkubwa kati ya Ilani ya uchaguzi ya CCM na bajeti ya wizara ya Ujenzi kuhusu Ujenzi wa barabara ya Tanzam.

Ilani inasema upembuzi yakinifu umekamilika lakini waziri katika bajeti yake anasema upembuzi yakinifu utafafanyika mwaka ujao wa fedha, sasa tumwamini nani CCM au Serikali? Anauliza Dr Tulia ambaye pia ni naibu Spika wa bunge.

Chanzo: Bungeni
Kimeumana,
Wapinzani hawamo Bungeni,wamebaki wanajitekenya na kucheka wenyewe.
 
Ilani ilijaa uongo na udhandiki kuchamganya na unafki hivi iyo ilani si ndio ilisema itatengeneza ajira milion 8 ndani ya miaka mitano?

miaka 60 ya uhuru chama hicho hicho kimeshindwa kutengeneza ajira million 5 tu unaanzaje kuamini kuwa kitatengeneza ajira million 8 ndani ya miaka 5 hiyo ilani imejaa uongo.
 
Mbunge wa Mbeya mjini Dr Tulia Ackson amesema kuna mkanganyiko mkubwa kati ya Ilani ya uchaguzi ya CCM na bajeti ya wizara ya Ujenzi kuhusu Ujenzi wa barabara ya Tanzam.

Ilani inasema upembuzi yakinifu umekamilika lakini waziri katika bajeti yake anasema upembuzi yakinifu utafafanyika mwaka ujao wa fedha, sasa tumwamini nani CCM au Serikali? Anauliza Dr Tulia ambaye pia ni naibu Spika wa bunge.

Chanzo: Bungeni


Yaani bunge limepwaya mpaka spika na naibu ndiyo wanatoa hoja
 
Hivi Tanzania unatofautishaje Chama(Ccm) na Serikali?

Ni kitu kimoja chenye majina tofauti nanitategemea unatumia wapi na muda gani na wazungumza na nani?

Zaidi if I were to choose as to who must be trusted , ningechagua kuamini wizara(waziri) na sio hili zimwi ccm.
The so called Ilani, ni compilation ya politicians' lies.
 
Back
Top Bottom