Ze Rock
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 270
- 563
Wasaaalam wana JF!
Leo kwenye bunge, kipindi cha maswali na majibu kuna, mbunge alionyesha malalamiko ya ucheleweshwaji wa Mafao kwa wastaafu katika maeneo mbali mbali Tanzania. Katika kujibu Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira). Alijibu swali hilo kuwa wastaafu wanapata mafao yao ikiwa wametimiza vigezo vyote ikiwemo uwasilishwaji wa nyaraka zinazohitajika. Alisisitiza hili mara kadhaa.
Katika hali niliyopendezwa nayo, Nayo Naibu spika akaonyesha kuwa majibu yale bado yana uwalakini katika kuhakikisha wastaafu wanapata mafao yao kwa wakati, akasema ikiwa mtumishi alikuwa anachangia mfuko wa jamii kwa miaka yote hiyo je kuna ulazima gani mstaafu huyu aanze tena kukusanya document wakati, Wahusika (Mifuko ya jamii wana taarifa zote za mstaafu huyo) Badala yake mifuko ya jamii iangalie jinsi ya kuzikusanya taarifa hizo na mstaafu alipwe stahiki zake.
Hii point kwa kweli Naibu spika nakupongeza na umeonyesha utashi, nia njema ya kuwasaidia wastaafu na weledi wa kazi hasa kiti ulichokalia kama Naibu Spika (Muongoza Bunge ). Safi sana usiishie hapa, endelea kukazia kila patakapo pwaya kwa weledi mkubwa kwani uwezo unao.
UNAMUITA MSTAAFU, BADALA YA KUMSAIDIA ATULIE SASA ALE MATUNDA YAKE, MNAANZA KUMTUMA MARA HIKI MARA KILE ILI APATE MATUNDA YAKE... NOT FAIR
KIZURI KISIFIWE TU
#HojaZenyeTijaKwaTaifa
#KwaWatanzania