Dkt. Tulia Ackson: Ikiwa mtumishi alichangia mfuko wa jamii, kuna ulazima gani wa mstaafu kukusanya documents wakati wahusika wana taarifa zake zote?

Ze Rock

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
276
1,000
Wasaaalam wana JF!

Leo kwenye bunge, kipindi cha maswali na majibu kuna, mbunge alionyesha malalamiko ya ucheleweshwaji wa Mafao kwa wastaafu katika maeneo mbali mbali Tanzania. Katika kujibu Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira). Alijibu swali hilo kuwa wastaafu wanapata mafao yao ikiwa wametimiza vigezo vyote ikiwemo uwasilishwaji wa nyaraka zinazohitajika. Alisisitiza hili mara kadhaa.

Katika hali niliyopendezwa nayo, Nayo Naibu spika akaonyesha kuwa majibu yale bado yana uwalakini katika kuhakikisha wastaafu wanapata mafao yao kwa wakati, akasema ikiwa mtumishi alikuwa anachangia mfuko wa jamii kwa miaka yote hiyo je kuna ulazima gani mstaafu huyu aanze tena kukusanya document wakati, Wahusika (Mifuko ya jamii wana taarifa zote za mstaafu huyo) Badala yake mifuko ya jamii iangalie jinsi ya kuzikusanya taarifa hizo na mstaafu alipwe stahiki zake.

Hii point kwa kweli Naibu spika nakupongeza na umeonyesha utashi, nia njema ya kuwasaidia wastaafu na weledi wa kazi hasa kiti ulichokalia kama Naibu Spika (Muongoza Bunge ). Safi sana usiishie hapa, endelea kukazia kila patakapo pwaya kwa weledi mkubwa kwani uwezo unao.

UNAMUITA MSTAAFU, BADALA YA KUMSAIDIA ATULIE SASA ALE MATUNDA YAKE, MNAANZA KUMTUMA MARA HIKI MARA KILE ILI APATE MATUNDA YAKE... NOT FAIR

KIZURI KISIFIWE TU

#HojaZenyeTijaKwaTaifa
#KwaWatanzania
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
16,781
2,000
Mifuko haina pesa.

Lengo la kumpiga mtu tarehe, danadana na kumsumbua ni ili waendelee kukusanya kusanya.

Hakuna mstaafu anastaafu kwa bahati mbaya au kwa ghafla tu.

Mifuko inajua kabisa umri wa kustaafu ni miaka 55-60 na inajua wachangiaji wangapi watafikisha umri huo kwa mwaka husika.

Wewe hujiulizi kwanini wabunge wakimaliza miaka 5 tu faster wanabeba mafao yao. Hakuna kuzungushana.

Hizo nyingine ni drama na unafiki tu.
 
Ze Rock

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
276
1,000
Mifuko haina pesa.

Lengo la kumpiga mtu tarehe na kumsumbua ili waendelee kukusanya kusanya...
Lakini kwa mujibu wa majibu ya Naibu waziri hakuonyesha kama kuna upungufu wa fedha na alimuahidi mbunge mmoja ambaye ana watu wake jimboni kwake yapata miaka mitatu hajalipwa akamwambia wawasiliane ili wastaafu hao walipwe.

So nafikiri pesa zimetengwa na zipo na amini hivyo. Ebu tuangalie impact ya hizi hoja zenye nguvu kwa wakati huu na ujao. Then kuna muda tuta yajadiri kwa ufanisi na data vizuri. Tuwaache watendaji watende kwanza.
 
nsalu

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
803
1,000
Sijui Bunge litaanza lini kuonyeshwa live naona ni kipindi cha maswali na majibu tu kiisha basi matangazo ya live yanaondolewa.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
13,700
2,000
Mtu akistaafu anatakiwa kupewa pesa yake siku hiyohiyo. Maana wanaostaafu wanajulikana, ni suala la kuandaa suala lao mapema. Takwimu zote wanazo, walipokuwa wanachukua michango mbona walikuwa hawadai Nyaraka kila mwezi?
 
dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,011
2,000
Mimi nipo nahangaikia mirathi . yaani pesa zilizoachwa na marehemu kwenye akaunti kuzipata ni mbinde kwelikweli! Eti akaunti ya mahakama wakipokea pesa zinarudishwa hazina ndo zije kutumwa tena halafu ndo msimamizi wa mirathi uitwe na mahakama kuzichukua!

Yaani kero tupu
 
Torque vs HP

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
1,782
2,000
Lakini kwa mujibu wa majibu ya Naibu waziri hakuonyesha kama kuna upungufu wa fedha na alimuahidi mbunge mmoja ambaye ana watu wake jimboni kwake yapata miaka mitatu hajalipwa akamwambia wawasiliane ili wastaafu hao walipwe. So nafikiri pesa zimetengwa na zipo na amini hivyo. Ebu tuangalie impact ya hizi hoja zenye nguvu kwa wakati huu na ujao.... Then kuna muda tuta yajadiri kwa ufanisi na data vizuri... Tuwaache watendaji watende kwanza.
Unaongea kama umekalia kitu chenye ncha kali,watu miaka 3 hawajalipwa mafao yao na wewe unaongea kirahisi rahisi tu.
 
Ze Rock

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
276
1,000
sawa karani wa naibu spika
Tukiwa vijana katika Taifa tusiache kuzungumza mambo yenye tija kwa upana wake hii inasaidia kuimarisha mawazo chanya kwa Taifa letu kuliko kuwa na mawazo kama haya, yaani sisi vijana tu tunaonyesha kutokomaa vema kwenye kuinua hoja zenye tija unategemea mwanasiasa akishaona haya, anajua kabisa vijana na wa pool table na viduku kesho ukitoa wazo lenye tija faili lako linakuchafua then kilio kina Anza, tumepewa wasaha wa kutoa mawazo chanya kwa maslai ya Taifa so tutumie vema
 
Torque vs HP

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
1,782
2,000
Mifuko haina pesa sababu imejiingiza kwenye uwekezaji usio na tija kwa wastaafu, ukisoma ripoti ya cag utaona jinsi pesa za mifuko zilivyopotea kwenye miradi kama ya uanzishaji viwanda vya sukari, ujenzi wa majengo na miradi mingine
Na jamaa alikua anajua fedha za wastaafu ndio maana ya fedha za ndani a.k.a nchi hii ina mapesa mengi a.k.a ni donor country.
 
Torque vs HP

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
1,782
2,000
Tukiwa vijana katika Taifa tusiache kuzungumza mambo yenye tija kwa upana wake hii inasaidia kuimarisha mawazo chanya kwa Taifa letu kuliko kuwa na mawazo kama haya, yaani sisi vijana tu tunaonyesha kutokomaa vema kwenye kuinua hoja zenye tija unategemea mwanasiasa akishaona haya, anajua kabisa vijana na wa pool table na viduku kesho ukitoa wazo lenye tija faili lako linakuchafua then kilio kina Anza, tumepewa wasaha wa kutoa mawazo chanya kwa maslai ya Taifa so tutumie vema
Utaahira mtupu unaandika hapa.
 
Ze Rock

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
276
1,000
Unaongea kama umekalia kitu chenye ncha kali,watu miaka 3 hawajalipwa mafao yao na wewe unaongea kirahisi rahisi tu.
Ndiyo maana waziri mwenye dhamana amekubali mabadiliko hayo na ameonyesha moyo wa kusaida hili. Ebu vijana twende na wakati tuache ile tabia ya kukariri vitu itapendeza zaidi. Lengo ni kupaza sauti na kuhakikisha mabadiliko yenye Tija yanakamilika na watu wana nufaika na sauti zenye mlengo wa kusaidia watu wenye vikwazo ktk nyanja mbali mbali.
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
3,649
2,000
Tukiwa vijana katika Taifa tusiache kuzungumza mambo yenye tija kwa upana wake hii inasaidia kuimarisha mawazo chanya kwa Taifa letu kuliko kuwa na mawazo kama haya, yaani sisi vijana tu tunaonyesha kutokomaa vema kwenye kuinua hoja zenye tija unategemea mwanasiasa akishaona haya, anajua kabisa vijana na wa pool table na viduku kesho ukitoa wazo lenye tija faili lako linakuchafua then kilio kina Anza, tumepewa wasaha wa kutoa mawazo chanya kwa maslai ya Taifa so tutumie vema
naona unataka kupita bila kupingwa,yote ni siasa na yanatija itategemea unalenga nini hasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom